
Jamaa aliyejitambulisha kama Kevin Prince Onyango (25) kutoka Homa Bay alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Irene Adhiambo (23) ambaye alitengana naye hivi majuzi.
Kevin alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja uliharibika baada ya babake Irene kumlazimisha kutengana naye ili kuolewa na mwanaume mwingine tajiri.
"Nilikuwa na mchumba. Tulikuwa tunapendana, tulikuwa poa. Ilianza wiki jana Jumatatu, babake alimwambia kuna rafikiye alikuwa anataka msichana. Alimwambia aachane na mimi ati huyo jamaa ako na pesa," Kelvin alisimulia.
"Irene alisema sio kutaka kwake kuenda lakini ni vile analazimishwa. Anaogopa babake, sasa alisema anaona afanye tu vile babake anataka. Huyo jamaa ako na miaka kama 46. Huyo jamaa alikuwa na bibi. Bibi yake hakuwa anazaa, sasa alitaka Irene aende awe mke wa pili ili amzalie," aliongeza.
Kevin alisema mchumba wake tayari amekiri kwamba amekumbwa na msongo wa mawazo kutokana na hali hiyo.
"Msichana anaishi na babake Nairobi. Kuna siku ingine alinipigia akaniambia ako na stress.. Aliniambia ako na msongo wa mawazo juu babake amemwambia kama hatafanya hivyo atafute kwa kukaa. Mimi nilijaribu kumuongelesha, ndugu yake alimuongelesha, mamake pia alimuongelesha. Kutokana na msukumo alisema afanye tu vile babake anataka. Huyo jamaa alimueka hadi akablock number yangu," alisema.
Irene alipopigiwa simu, alidai kwamba yuko bize na hawezi kuzungumza sana.
Kevin alisema, "Kama uliamua hivyo, acha kuangalia nyuma. Kaa tu huko, ukae sawa. Mimi pia najiangazia, nikipata mwingine nitahukuru tu Mungu. Sina mengi ya kusema juu uamuzi ulishafanyiwa.."
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?