
Mwanadada aliyejitambulisha kama Caroline Kathambi mwenye umri wa miaka 29 kutoka Kayole alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Felix Omondi (40) ambaye alikosana naye miezi kadhaa iliyopita..
Caroline alisema uhusiano wake na Omondi wa miaka 8 uliharibika Desemba mwaka jana wakati mpenzi alikatiza mawasiliano naye baada ya kuenda nyumbani.
Aidha, alifichua kwamba kwa sasa ana ujauzito wa miezi 7, ambao alipata kinyume na matakwa ya mpenziwe.
“Mwezi Desemba mwaka jana nilikuwa naenda nyumbani Christmas. Wakati huo nilikuwa mgonjwa, na nilikuwa na mimba. Nikamwambia niende nikae nyumbani juu mambo si mazuri sana. Hatukuwa tunaishi na yeye awali. Tukaongea akasema ni sawa niende juu maisha Nairobi sio mazuri. Mimi nikaenda tu, ata hakunipea nauli. Nilienda nyumbani nikakaa,” Caroline alisimulia.
Caroline alifichua kwamba mara ya mwisho ambapo alipokea ujumbe kutoka kwa mpenziwe ilikuwa Desemba 18.
“Nikimtext ama kumpigia simu hashiki. Hivyo tu ndio alininyamazia imagine. Sasa tarehe 16 kumbe ilikuwa siku ya mwisho aliniongelesha. Aliniandikia tu meseji akaniambia maisha Nairobi ni ngumu sana ata hana chochote,” aliongeza.
“ Bado sijajifungia, niko na mimba ya miezi saba sasa. Meseji huwa anapokea vizuri lakini hawezi jibu, nikimpigia ni kama ameniblock. Tumekuwa na yeye miaka nane, lakini hatukuwa tunaishi pamoja. Tulikuwa tunapenda juu alikuwa anakuja kuniona ata kama sio kila siku,” alisema.
Omondi alipopigiwa simu alidai kwamba hamtambui Caroline kisha kukata simu mara moja.
“Simjui mtu kama huyo tafadhali,” alisema.
Caroline alisema, “Simu zangu huwa hashiki. Ata meseji huwa
hajibu. Alikuwa ameniambia hataki mimba. Labda shida ni hiyo. Mimi sijui
nilishika mimba aje, ata mimi mwenyewe sikuwa nataka pia na sikuwa natarajia… Ni
sawa tu hakuna njia nyingine. Nitakubali tu.”
Katika maneno yake ya mwisho kwa mpenziwe, Caroline alisema, “Felix
naomba tu kama nimewahi kukusea unisamehe. Tafadhali tu kwa ajili ya huyu
mtoto, unisaidie vile tutalea.”