In Summary

• Mwanamama huyo alisema wanawake wanaolenga kumtongoza mpenzi wake mpya Madini Classic, yeye hana haja wacha wajaribu bahati yao.

Pritty Vishy, Stevo Simple Boy na Madini Classic
Image: Instagram

YouTuber Pritty Vishy katika siku za hivi karibuni haswa baada ya aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Stevo Simple Boy kutangaza kwamba amepata mchumba na hata kumvisha pete hadharani, amekuwa akionekana kutomfurahikia Stevo kwa hatua zake na badala yake kueneza chuki kumhusu.

Siku chache zilizopita kupitia ukurasa wake wa Instagram alikuwa na kipindi cha moja kwa moja kujibu maswali ya mashabiki wake. Wengi walionekana kumuuliza maswali kuhusu uhusiano wake na Stevo Simple Boy haswa baada ya kila mmoja kumtambulisha mpenzi wake mpya.

Vishy alidhihirisha wazi chuki yake dhidi ya Simple Boy kwa kuonekana kumdhihaki katika kile kilichoonekana kuwa ni uchungu alio nao kwa kuachana na msanii huyo wa kibao cha ‘Freshi Barida’

Katika moja ya maswali, mmoja alitaka kujua mawazo yake kuhusu muonekana mpya wa msanii huyo. Juzi Stevo alipakia picha maridhawa wikendi iliyopita akiwa na suti ya kufana huku akidokeza kwamba anatarajia kufunga nikaha na mchumba wake Gee hivi karibuni.

Vishy kwa kejeli alionekana kurusha tope katika uvaaji huo wa Simple Boy huku akionekana kumshambulia na kujitenga na kumzungumzia kwa wakati mmoja.

“Sijasema ati ooh amekaa vibaya lakini heeh Mungu anaona mweney alimvalisha,” Vishy alitoa kauli hii ambayo wazi inaonesha hakuwa anafurahia muonekano wa Simple Boy.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa wanadada wengine ambao wanamfuata mpenzi wake mpya kwenye DM na kujaribu kumtongoza, mwanadada huyo aliwashangaza wengi aliposema kwamba wanadada hao kama wapo waendelee tu kujaribu bahati yao. Alifafanua kwamba yeye kazi yake si kumchunga Madini Classic kutokana na wanawake wanaomtongoza DM.

“Kwani mimi nafaa kushughulika na wao? Acha wajaribu bahati yao kwa sababu mimi ni kazi yangu kuchunga mwanaume,” Pritty Vishy alijibu.

Vishy aliwahi nukuliwa katika mahojiano na mchekeshaji Dr. Ofweneke akisema kwamba Madini asipocheza nafasi yake kama mchumba basi hataona hatari ya kumsaliti kimapenzi.

Baada ya kujulishwa kwamba Stevo Simple Boy anapanga kufanya harusi na mpenzi mpya hivi karibuni na kuulizwa iwapo atahudhuria, Vishy alikataa kabisa. Sababu yake ya kutohudhuria ni hangetaka kumchanganya Simple Boy kwa maungo yake ya kudumu ambayo yanaweza mfanya asizingatie kile mhubiri atakuwa anawausia kuhusu ndoa.

View Comments