NI Rasmi sasa kwamba mwanamitindo Hamisa Mobetto na mwanasoka Stephane Aziz Ki ni mtu na mkewe baada ya wawili hao kukamilisha taratibu zote za ndoa.
Mwanamitindo huyo, mama wa watoto wawili alifunga harusi na
Stephane Aziz Ki, mchezaji wa Klabu ya Yanga nchini Tanzania ambaye ni raia wa
Burkina Faso, Afrika Magharibi.
Aziz Ki alilipa mahari na sasa mamake Mobetto asmefichua
idadi ya ng’ombe ambao mchezaji huyo alitoa.
Akizungumza na Zamaradi TV katika mahojiano ya baada ya
shughuli, mamake Hamisa Mobetto alisema kwamba ng’ombe ambao mchezaji huyo
alitoa kama mahari ni 150 pamoja na kiasi cha pesa nyingi.
Mama mtu alisisitiza kwamba ng’ombe hawakuwa 30 kama ambavyo
baadhi ya watu walijaribu kusema mitandaoni, akisema kuwa malori yaliyokuwa
yamebeba ng’ombe hao yalipiga foleni hadi nyumbani kwake.
“Nadhani ilikuwa
mubashara jamani kila mtu ameona ng’ombe wale wamesimama. Ng’ombe walikuwa nadhani
malori mawili na walienda kwa mamangu.”
“Sijawahesabu kwa sababu
unajua nilikuwa kwenye furaha na mihemko lakini ng’ombe tuliokubaliana nao ni
100. Unajua ng’ombe mmoja mzima ni shilingi milioni 3.5. lakini wao walileta ng’ombe
kama 150, wengine walipelekwa kwa mama, wale walioonekana pale ni wachache,’ alisema.
Mama huyo alisema kwamba yeye ametoka katika familia ya chifu
na kwao ni sheria mahari kulipwa kwa kutumia ng’ombe walio hai.
“Kwa hiyo wao walileta ng’ombe 150 na kiasi cha pesa ambacho
siwezi kukitaja,” mama mtu alisisitiza.
Awali, kulikuwa na taarifa kwamba Aziz Ki alilipa jumla ya ng’ombe
30.
Wakati wa hafla hiyo, Hamisa Mobetto alisema anamshukuru Mungu kwa kumpa mpenzi
anayemuona kuwa ndiye sahihi kwake na sasa rasmi ni mchumba wa mtu anayempenda
kwa dhati.