logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harusi Tunayo! Mipango Ya Harusi Ya Hamisa Mobetto na Mwanasoka Aziz Ki Yafichuliwa

Wawili hao walianza kuonekana pamoja mapema mwaka jana kabla ya kuthibitisha mahusiano mapema mwaka huu.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku11 February 2025 - 07:57

Muhtasari


  • Mwanamitindo Hamisa Mobetto na mchezaji wa soka kutoka Burkina Faso, Stéphane Aziz Ki, wamefichua mipango yao ya harusi.
  • Wawili hao walitangaza kuwa sherehe za harusi yao zitafanyika kwa siku tatu, kuanzia Februari 15, 2025.

Hamisa Mobetto Na Aziz Ki

Mwanamitindo na mfanyabiashara mashuhuri wa Tanzania, Hamisa Mobetto na mchezaji wa soka kutoka Burkina Faso, Stéphane Aziz Ki, wamefichua mipango yao ya harusi.

Wawili hao walitoa tangazo hilo la kusisimua kupitia mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu na limepokewa kwa shangwe na mashabiki wao.

Hamisa na Aziz Ki walianza kuonekana pamoja mara kwa mara mapema mwaka jana na tangu wakati huo, wamekuwa wakionyesha waziwazi dalili kuwa wao ni wapenzi.

Kupitia chapisho la pamoja kwenye Instagram, wawili hao walitangaza kuwa sherehe za harusi yao zitafanyika kwa siku tatu, kuanzia Februari 15, 2025 ambapo mahari italipwa.

Siku nyingine za hafla hiyo ni Februari 16 na Februari 19 ambapo kutakuwa na hafla za Nikkah na sherehe za harusi mfululizo, na zinatarajiwa kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka sekta mbalimbali, wakiwemo wasanii, wanamichezo, na wafanyabiashara wakubwa kutoka Afrika na kwingineko.

Tangazo hili linakuja miezi michache baada ya Hamisa kumaliza uhusiano wake na mfanyabiashara wa Togo, Kevin Sowax.

Mnamo Mei 2024, mpenzi huyo wa zamani wa staa wa Bongo Diamond Platnumz alithibitisha kupitia mazungumzo na mashabiki wake kwenye Instagram kuwa alitengana na Sowax kutokana na changamoto za umbali na ratiba zao zenye shughuli nyingi.

Kabla ya mahusiano yake na Aziz Ki na Sowax, Hamisa pia aliwahi kuhusishwa kimapenzi na rapa wa Kimarekani, Rick Ross, ingawa hakukuwa na uthibitisho wa wazi kuhusu uhusiano huo.

Mashabiki wa Hamisa na Aziz Ki wameonyesha msisimko mkubwa baada ya tangazo hilo, wakijaza mitandao ya kijamii kwa pongezi na jumbe za heri njema kwa wanandoa hao watarajiwa.

Wengi wanaamini kuwa harusi hii itakuwa moja ya sherehe kubwa zaidi katika tasnia ya burudani Afrika mwaka huu.

Kwa sasa, maandalizi yanaendelea huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona jinsi hafla hii itakavyofanyika.

Itabaki kuwa moja ya harusi zinazotarajiwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa burudani na mitindo barani Afrika.

Hamisa pia aliwahi kuchumbiana na Diamond Platnumz takriban miaka minane iliyopita na waliaminika kupata mtoto pamoja. Hata hivyo, suala la mtoto ambaye Hamisa alijifungua wakati wa mahusiano yao limebaki kuwa tata.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved