
WINNIE Byanyima, mke wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye na ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa zamani war ais Yoweri Museveni amemuonya mwanawe rais huyo, Muhoozi Kainerugaba dhidi ya kuzungumzia uhusiano huo wa zamani, akisema hajui chochote.
Kupitia ukurasa wake wa X, Byanyima
alimuonya Muhoozi dhidi ya kukurupukia na kupayukia suala la uhusiano wake wa
zamani na Museveni, akisema kwamba ni uhusiano uliokuwa changamano zaidi na
ambao wote – yeye na Museveni, waliamua kuutupa katika kaburi la sahau na kila
mmoja kujishughulisha na ya kwake.
"@mkainerugaba IWE MWANA WE….
Yetwaare. Ninahisi ni muhimu kuwa wazi: Kuna historia ngumu zaidi kati ya baba
yako na mimi ambayo sote tumechagua kuvuka kwa kuheshimiana," Byanyima alichapisha kwenye X.
Winnie alimuonya Muhoozi zaidi akisema
kwamba ikiwa ataendelea kuzungumzia uhusiano wake wa zamani na Museveni basi
itambidi atoe ukweli mgumu ambao utamchanganya na kumfanya kujuta.
"Hata hivyo, ikiwa utaendelea
kuwasilisha simulizi ya uwongo, huenda nikahitaji kutoa ushahidi MGUMU wa
ukweli. Napendelea kudumisha mtazamo wetu wenye heshima, lakini chaguo hilo
linabaki kuwa lako. Ninaona kuwa suala hili limefungwa."
Jenerali Kainerugaba, ambaye ni Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi, alienda kwa X kusimulia jinsi uhusiano kati ya Museveni na
Byanyima ulivyomalizika.
Muhoozi alitoa tamko lake saa chache baada
ya Winnie kudai kwamba katika kitabu chake kijacho, atasimulia kwa sehemu
kuhusu uhusiano wake wa zamani na Museveni kabla ya kuachana na kuoana na
Besigye.
"HAKUNA kitu cha kawaida katika
uhusiano wako na baba yangu. Ulipata nyumba yenye furaha ukajaribu kuibomoa.
Wewe ni MSIBA wa mwanamke!! Hukutoka. Mzee alikufukuza nyumbani Desemba 1986,
akakuburuza hadi kwenye gari huku unalia na kukupeleka kwa wazazi wako."
Kabla ya kufunga ndoa na Dk Kizza Besigye
Julai 7, 1999, huko Nsambya, Kampala, Byanyima alikuwa akihusishwa kimapenzi na
Museveni. Yeye na Besigye wana mtoto wa kiume, Anselm Besigye, ambaye kwa sasa
anafuata PhD katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York.