
Msanii maarufu wa Marekani, Snoop Dogg, mnamo siku ya Jumatatu alizua msisimko mkubwa miongoni mwa Wakenya baada ya kuchapisha video ya Naibu Rais wa zamani, Rigathi Gachagua, kwenye akaunti yake ya Instagram.
Video hiyo, iliyorekodiwa wakati wa kikao cha Gachagua na wanahabari cha awali, inamuonyesha naibu rais huyo aliyetimuliwa akipitia kurasa za kijitabu, kitendo ambacho Snoop Dogg alikitumia kuongeza ucheshi kwenye ukurasa wake.
Katika chapisho hilo, rapa huyo aliandika maneno "Looking for the part of the story that says I am the one to play with," akimaanisha anatafuta sehemu ya hadithi inayosema yeye ndiye wa kuchezea.
Chapisho hili lilivutia maelfu ya Wakenya ambao walifurika kwenye sehemu ya maoni, wakionyesha msisimko na mshangao wao kwa kuona mwanasiasa wao akipata umaarufu wa kimataifa kupitia njia isiyotarajiwa.
Video ambayo Snoop Dogg alichapisha ilirekodiwa wakati wa mahojiano ambayo Gachagua alifanya katika makazi yake ya zamani katika mtaa wa Karen, Nairobi.
Mahojiano hayo yalifanyika siku moja kabla ya naibu rais huyo wa zamani kufika katika Bunge la Kitaifa kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja ya kumngβoa madarakani.
Baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa Instagram yalionyesha uzalendo na ucheshi wa hali ya juu..
"Kenya hoyeeeee ππππ Riggy G ametufikisha hapa π°πͺπ°πͺπ°πͺπ°πͺ," mtumizi mmoja wa Instagram aliandika, kionyesha furaha yake kwa Gachagua kufikia kiwango hicho cha kutambulika.
Mwingine alitania, βHakuna comment ya English huku ππππ π°πͺπ°πͺπ°πͺπ°πͺ,β akibainisha jinsi Wakenya walivyotawala sehemu ya maoni kwa lugha yao ya taifa.
Pia, baadhi ya watumiaji wa mtandao waliona tukio hili kama fursa ya kumwalika Snoop Dogg nchini Kenya.
"Snoop, unapaswa kuja Kenya sasa. Tunakupenda hapa!" mwingine aliandika.
Hii inaonyesha jinsi Wakenya wanavyothamini na kufurahia utamaduni wa kimataifa na wanavyopenda kutangamana na wasanii maarufu kama Snoop Dogg.
Tukio hili limeonyesha jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kuunganisha tamaduni tofauti na kuleta umaarufu kwa watu kupitia njia zisizotarajiwa.
Pia, limeonyesha ucheshi na mshikamano wa Wakenya katika kusherehekea matukio yanayowahusu viongozi wao, Wakenya wenzao, na nchi yao kwa ujumla.