
MBUNGE wa Mumias Mashariki. Peter Salasya ameweka wazi kwamba mazingira ya nyumbani kwake katika kaunti ya Kakamega ni safi licha ya kutokuwa na mke.
Mbunge huyo mcheshi ambaye katika siku za hivi karibuni
amekuwa mwiba mchungu kwa kinara wa ODM Raila Odinga alisema haya wakati
alikuwa akimkaribisha nyumbani kwake kijana ambaye alichangia pakubwa kampeni
zake kwa kutunga wimbo ambao anahisi ndio uliwachochea wapiga kura kukubali
sera zake.
Alisema kwamba kijana huyo alipata changamoto kuona nyumbani
kwake ni safi na nadhifu licha ya mbunge huyo kutokuwa na mke.
Hata hivyo, Salasya alifichua kwamba ako na kijana wa kiume
ambaye anamsaidia katika usafi wa nyumba yake.
“Mwanamuziki alishangaa
kupata nyumba iliyopangwa vizuri isiyo na mke hehe ingawa nilimpa changamoto
niko na house boy anafanya kazi ya ajabu,” Salasya alieleza.
Katika kipindi cha siku za hivi majuzi, Mbunge huyo amekuwa
akikashifu ubia mpya baina ya rais William Ruto na kinara wa Azimio Raila
Odinga.
Salasya hata hivyo amejipata akiburuzana mabega na baadhi ya
wafuasi wa viongozi hao wawili, jambo ambalo hajalikalia kizembe.
Katika chapisho kwa njia ya video, Salasya aliwataka watu
ambao bado wanaunga mkongo Raila Odinga kusitisha ufuasi katika kurasa zake za
mitandao, akisisitiza haja ya kuwa na wafuasi wachache ambao wanafuata miongozo
yake.
“Kama wewe ni mtu wa
nyanza ama mufuasi wake na unaona sikubambi ebu unfollow me right now because
you won’t have peace nitakupa depression. Nataka kubaki na wafuasi wachache
ambao tunashiriki ideology ya kawaida ...lazima niwatoe ujinga wa huyu baba
yenu ambaye amebadili akili zenu. Ametuchezea muda mrefu na lazima tumchezee
sasa hivi,” Salasya alifoka.
Mbunge huyo hata alisema kwamba yuko tayari kupokea madhara
yoyote yatakayotokana na msimamo wake wa kupinga ubia wa UDA na ODM.
Alisema kuwa haogopi kutolewa katika serikali hiyo jumuishi,
akisema lengo ni kuhakikisha wananchi wanafahamu kile alichokitaja kama ukweli.