
SEHEMU ya vijana katika kaunti ya Nandi wametupa lawama zao za kushindwa kupata wenzi wa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi nao kwa kile wanahisi ni ukosefu wa huduma nzuri ya mawasiliano.
Katika simulizi hiyo ya kustaajabisha iliyoandaliwa na
runinga ya NTV Kenya, baadhi ya vijana na wazee walionekana kupata sababu ya
kukosa kupata wapenzi, wakisema kwamba huduma ya mawasiliano ni duni.
“Ukitembea karibu kila
kijiji unapata vijana wengi hawajaoa na wengine hawajaolewa, shida ni hii
network, kutafutana kwa simu ni ngumu, mawasiliano hakuna,” alisema Caren Komen,
mkaazi wa kijiji cha Chebarus.
“Hata vijana siku hizi
vile wanataka kuoa kupata mawasiliano na wenzao ni ngumu kwa maana hana network
nzuri ya kuwasiliana naye,” Joseph Sitienei, mzee katika kijiji
hicho aliongeza.
Wengine hata walidai kwamba huduma za mawasiliano ni duni
kiasi kwamba mtu hawezi hata tumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na wenzake.
Walihisi kwamba wakati wengine wanatumia muda wao kutangamana
na wenzao kwenye mitandao ya kijamii, vijana wa eneo hilo wengi hupata starehe
yao kwa matumizi ya dawa za kulevya.
“Network hapa ni duni
sana, huwezi ingia hata Facebook. Kwa hiki kijiji vijana wako wengi, wamesema lakini
kazi yao sasa hivi wakipata pesa ni kuvuta sigara, kunywa pombe, bangi wanatumia
kwa sababu wamezembea tu. Ndio tunataka tukomeshe huo uzembe tukipata network
nzuri. Mtu akuwe active kwa simu afanye kazi,” mwingine alisema.
Wakaazi hao walitoa wito kwa Idara husika kuwasaidia kupata
mawasiliano mazuri ili kuweza kuwasiliana na wenzao na hata kupata kazi za
mitandaoni.
“Tuko na mbegu tuseme
kama za kahawa hivi lakini tunakosa mtu wa kuuzia. Hivi kama tungekuwa na
network tunaweza fanya biashara ya kuuza mitandaoni mtu unachapisha watu
wanaona, lakini sasa hakuna, network ndio inatusumbua,” mwingine aliongeza.
Tazama simulizi hiyo hapa;