
JENERALI Mkuu wa majeshi ya Uganda, Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa rais Yoweri Museveni amemtaka rapa maarufu wa Marekani, Jay Z kufika Uganda kwa lengo la kumuomba msamaha.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa majeshi mbwatukaji, Jay Z ana kila
sababu ya kufika Uganda mara moja na kumuomba Muhoozi msamaha kwa kile
alichosema ni kosa la kumuona malkia wa muziki, Beyonce.
Muhoozi alikariri kwamba Beyonce ni mwanamke wake na Jay Z
kumuoa ilikuwa moja ya ukiukaji mkuu wa sheria ya Muhoozi, hivyo ana deni la
msamaha kwake.
“Jay-Z lazima aripoti nchini
Uganda na kuomba msamaha kwa kuoa mwanamke wangu...Beyonce,” Jenerali Muhoozi Kainerugaba
alichapisha kupitia X.
Aidha, mwanawe Museveni alisema kwamba ikliwa Jay ZX hatoweza
kutii amri hiyo, basi atangaza vita asubuhi na ikiwa Muhoozi ataibuka mshindi,
zawadi yake itakuwa kumchukua Beyonce kutoka kwake.
“Ninampa changamoto Jay-Z
kwenye pambano alfajiri. Nikishinda namchukua Beyonce. Huyu jamaa amenivuruga
vya kutosha!” Muhoozi Kainerugaba aliongeza.
Hii si mara ya kwanza kwa Muhoozi kuonekana kummezea mate
Beyonce, mama wa watoto 3 ambaye amekuwa katika ndoa na Jay Z tangu mwaka 2008.
Wanandoa hao walifunga pingu za maisha katika sherehe ya siri
mnamo Aprili 4, 2008, kwenye jumba la kifahari la Jay-Z la Manhattan,
lililopambwa kwa maua 70,000 ya dendrobium.
"Ilikuwa harusi ya
kihisia-moyo-kilio sana-na kwa kweli kiroho," chanzo kiliambia People
wakati huo.
Wana watoto watatu: binti Blue Ivy, aliyezaliwa mnamo 2012,
na mapacha Rumi na Sir, waliozaliwa mnamo 2017.
Walichumbiana kwa takriban miaka saba kabla ya kuoana, huku
Beyoncé akisema kuwa aliona ni muhimu kujijua na kuwa na maisha yake kabla ya
kujitoa kwenye ndoa.
Kwa upande mwingine, Kainerugaba amekuwa akijipaisha kuwa
shujaa wa Wamarekani weusi, huku pia akisema kwamba Wamarekani weusi watampa
heshima kwa kuita wanao kwa jina lake.
“Nitakuwa shujaa MKUBWA
zaidi kwa Wamarekani Weusi! Dada zangu weusi nchini Marekani watawapa watoto
wao majina yangu,” Kainerugaba alijitapa.