
MWANAMUME mwenye umri wa makamo amewazuzua watumizi wa mitandao wa TikTok baada ya kunaswa kwenye video akiwa katikati ya barabara na bango la kuomba msaada.
Kwa kawaida, watu wengi hujitokeza na
mabango kwenye makutano ya barabara zenye shughuli nyingi yakiwa na jumbe za
kuomba msaada kuhusu masuala kama matibabu, ufadhili wa elimu… lakini jamaa
huyu alikuwa anaomba msaada ya kupewa gari.
Kilichowashangaza wengi, jamaa huyo alikiri kwamba alikuwa na kazi na gari lingemlrahisishia kazi yake.
“Mungu tafadhali gusa mtu yeyote wa
kunibariki na gari kwa ajili ya kazi yangu,” Jamaa huyo aliandika
kwenye bango lake akifuatisha na nambari ya simu.
Watu walitoa maoni mbalimbali, baadhi
wakikashifu kile walichoita kutumia suala la omba-omba visivyo na kumtaka
kuridhika na kazi kwani kunao wengi wasio hata na hiyo kazi na ndio wanastahili
kusaidiwa.
Wengine pia walionekana kukinzana na
dhana ya kumsaidia mtu maskini, wakisema kwamba mtu anasaidiwa na baadae kuwa
jeuri kwani hakupitia ugumu kutajirika bali kupitia njia ya misaada.
Haya hapa ni baadhi ya maoni;
"Hakuna kitu kinachoumiza kama
kuinua maskini ambaye siku moja atakumeza kabisa kwa sababu hawakukulazimisha
kuwasaidia .....mimi Ama ... kamwe tena."
"Hakuna mtu anayepaswa kujaribu
hii. kama mmiliki wa gari utajuta sana. Moja ya majuto yangu maishani ilikuwa
kununua gari kwa mtu wa kufanya naye kazi." Mwingine alisema.
Eben alisema: "Nilichonifanyia
rafiki yangu mwenyewe 😭😭😭😭😭 nilikuwa nikifikiria
nilikuwa nikimsaidia bila kujua kwamba alitaka kunipeleka kwenye kaburi langu
la mapema 🪦 hmmmmmm mimi kamwe
hakuna mtu anayepaswa kujaribu kwamba utalia kama utafanya."