logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Familia ya Mwanahabari Sophie Ikenye yaomba msaada wa pesa za Matibabu

Familia ya mwanahabari Sophie Ikenye inaomba msaada wa pesa baada ya kutumia hela zote kwa ajili ya Matibabu hospitalini.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri24 March 2025 - 17:00

Muhtasari


  • Katika ombi la msaada wa pesa lililotumwa kwa umma ili kusaidia katika  ,michango  ya pesa za matibabu, familia iliweza kusema kuwa kwa zaidi ya miezi minane ambayo Sophie amekuwa hospitalini  waliweza kutumia hela zote.
  • Sophie ambaye alianza taasinia yake ya uanahabari kama mwanahabari wa masomo ya nyanjani pale KBC, akafanya kazi katika shirika la Royal media baadaye Nation media na sasa yuko BBC  Katika kipindi cha Focus on Africa on BBC HABARI ZA Ulimwengu.

Familia ya mwanahabari Sophie Ikenye inaomba msaada wa pesa baada ya  kutumia hela zote kwa  ajili ya Matibabu hospitalini.

Katika ombi la msaada wa pesa lililotumwa kwa umma ili kusaidia katika  ,michango  ya pesa za matibabu, familia iliweza kusema kuwa kwa zaidi ya miezi minane ambayo Sophie amekuwa hospitalini  waliweza kutumia hela zote.

Kulingana na taarifa ya Phillip Etale waliweza kukadiria bili ya  pesa zinazohitajika kama shilingi milioni tano,kulingana na familia imekuwa  ikisaidia na kulipa bili za matibabu kwa zaidi ya miezi minanae.

Sophie ambaye alianza taasinia yake ya uanahabari kama mwanahabari wa masomo ya nyanjani pale KBC, akafanya kazi katika shirika la Royal media baadaye Nation media na sasa yuko BBC  Katika kipindi cha Focus on Africa on BBC HABARI ZA Ulimwengu.

katika wito wa kuomba msaada wa pesa familia ilisisitiza kuwa kwa sasa haina  pesa ambazo zitamtibu mwanao ikikusudiwa kuwa anahitajika kufanyiwa upasuaji.

Famili pia iliweza kurai umma kwa msaada wowote ule utakuwa wenye tija kuu na kusema kuwa hata msaada wa ,maombi pia utakuwa wenye umuhimu mkubwa sana kwao.

Sophie alipata ajira BBC baada ya kupokea tangazo ambalo lilikuwa limetangaza nafasi ya ajira ambapo shirika hilo lilikua likihitaji ripota kutoka Afrika ukanda wa mashariki, magharibi na kusini mwa afrika ambapo aliibuka kama mtangazaji bora na kupata ajira.

Ulipofika mwaka wa 2009 aliweza kupewa kitengo maalum kama mwanahabari mwendesha vipindi hasa kipindi cha Angaziia Afrika( Focus on Africa) katika upande wa radio baada ya miaka mitatu kipindi hicho kiliweza kupeperushwa hewani kwa rininga.

 Katika safari yake kama mwanahabari Ikonye aliweza kuangazia matukio mbalimbali katika bara  la Afrika ikiwemo na tukio la mwaka 2011 katika uchaguzi mkuu nchini Naijeria  na masaibu kule Libya na uchaguzi mkuu nchini Kenya wa mwaka wa 2013.

Katika  safari yake aliweza kuwahoji zaidi ya Marais 10 wa bara la Afrika kuashiria kuwa amepiga hatua kubwa sana katika sanaa ya uanahabari na kumpa sifa nyingi ambazo atasalia kukumbuka daima.  

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved