
MUHOOZI Kainerugaba, mwanawe rais Yoweri Museveni ambaye pia ni jenerali mkuu wa majeshi ya Uganda, UPDF amejitokeza kwen ye mitandao wa X kama kawaida yake na kudai kwamba rais wa Marekani Donald Trump anamsikliliza.
Hii ni baada ya balozi wa Uganda katika baraza la Umoja wa
Mataifa, Adonia Ayebare kufichua kwamba serikali ya Marekani imerejesha misaada
ya matibabu ya virusi vya HIV nchini Uganda.
Kainerugaba alidakia taarifa hiyo na kusema kwamba Marekani
ilirejesha msaada wa matibabu ya UKIMWI Uganda kufuatia tweet yake siku chache
nyuma akimtaka Trump kufanya hivyo.
“Ninataka kumuambia rais
Donald Trump kurudisha msaada wa Marekani kwa wanaoathirika na virusi vya HIV
nchini Uganda. Watu wetu watashukuru sana,” tweet hiyo ya Muhoozi
siku 5 zilizopita ilisomeka.
Kama sadfa vile, balozi huyo alifichua taarifa kwamba hatimaye Marekani imerejesha msaada huo kwa Uganda, Muhoozi alimshukuru balozi huyo kwa kuhakikisha hilo lakini pia akamshukuru Trump kwa kusikiliza ombi lake la awali.
“Nimefahamu kutoka kwa Balozi @adoniaayebare kwamba serikali ya Marekani imerejesha usaidizi wote wa VVU/UKIMWI kwa Kituo cha Utafiti wa Kitabibu cha Pamoja (JCRC) baada ya tweet yangu siku chache zilizopita. Namshukuru Rais @realDonaldTrump na serikali yake kwa kuwa upande sahihi wa historia na kusaidia watu wetu! Pia nashukuru @USAmbUganda William Papa kwa kazi yake nzuri katika kurejesha usaidizi huu. Mwisho namshukuru Balozi @adoniaayebare kwa kuratibu juhudi hizi,” Muhoozi Kainerugaba alisema.
Mkuu huyo wa majeshi amekuwa mtu mwenye misimamo ya ajabu
kupitia tweet zake katika mitandao wa X, huku akimshambulia mtu yeyote kwa wakati
wowote anaoutaka yeye.
Wiki chache zilizopita, Muhoozi alikuwa akishambuliana na
aliyekuwa mpenzi wa ujanani wa babake, Winnie Byanyima – ambaye sasa ni mke wa
mwanasiasa wa upinzani Kizza Besigye.
Wiki hii, Muhoozi amekuwa akishambulia moja ya gazeti maarufu
la humu nchini baada ya jarida hilo kuchapisha stori yake kwenye ukurasa wa
mbele katika moja ya toleo la wikendi iliyopita.