logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaharakati maarufu wa mtandaoni Jumuiyan afariki kwa kujitoa uhai, aacha barua

Kwa mujibu wa polisi, Jumuiyan, mwenye umri wa miaka 31, aliacha barua ya kuaga kabla ya kufariki.

image
na CYRUS OMBATIjournalist

Dakia-udaku29 March 2025 - 12:50

Muhtasari


  • Mwili wake ulipatikana ndani ya nyumba yake mnamo Machi 26, katika tukio lililoripotiwa kutokea saa nne usiku, baada ya kudaiwa kumeza sumu.
  • Jumuiyan alikuwa kipenzi cha jamii ya mtandaoni, akijulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya utawala mbaya.

Mwanaharakati mashuhuri wa mtandaoni, James Musa Awandu, maarufu kama Jem Guru au Jumuiyan

Mwanaharakati mashuhuri wa mtandaoni, James Musa Awandu, maarufu kama Jem Guru au Jumuiyan, amefariki kwa madai ya kujiua katika nyumba yake katika eneo la Ngong, Kaunti ya Kajiado.

Kwa mujibu wa polisi, Jumuiyan, mwenye umri wa miaka 31, aliacha barua ya kuaga kabla ya kufariki.

Mwili wake ulipatikana ndani ya nyumba yake mnamo Machi 26, katika tukio lililoripotiwa kutokea saa nne usiku, baada ya kudaiwa kumeza sumu.

Inaripotiwa kuwa kabla ya tukio hilo, alimpigia simu msimamizi wa jengo lake akiomba msaada. Hata hivyo, juhudi za kumuokoa hazikufanikiwa.

Polisi walipofika katika nyumba aliyokuwa akiishi peke yake, walikuta vyombo vinavyoshukiwa kuwa na mabaki ya sumu aliyotumia pamoja na barua ya kuaga iliyokuwa kwenye meza.

Maafisa wa uchunguzi wanachambua barua hiyo ili kuthibitisha uhalisia wake, na wameeleza kuwa itapelekwa kwa mtaalamu wa maandishi kwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo, polisi hawajafichua yaliyomo kwenye barua hiyo huku uchunguzi ukiendelea.

Mwili wake ulihamishiwa katika hifadhi ya maiti, ambako upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanyika Ijumaa ili kubaini chanzo halisi cha kifo chake.

Habari za kifo chake ziliwashtua marafiki na familia yake katika eneo la Kibaoni, Kaunti ya Kilifi, ambao sasa wanaomba msaada wa kifedha ili kugharamia mazishi yake.

Jumuiyan alikuwa kipenzi cha jamii ya mtandaoni, akijulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya utawala mbaya.

Wengi walimtaja kama “captain” wa harakati za mtandaoni kutokana na ujasiri wake na uwezo wa kueleza mawazo kwa ucheshi na weledi, hasa kwenye jukwaa la X.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa miongoni mwa wafuasi wake na wanaharakati wenzake.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved