logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Haikuwa rahisi, lakini ilikuwa bora!" Mpenziwe Eric Omondi afichua sababu ya kumaliza uhusiano wao

“Nimechukua uamuzi wa kumaliza uhusiano wangu na Eric Omondi," Lynne alitangaza.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku09 April 2025 - 09:40

Muhtasari


  • Lynne alitoa taarifa ya kushangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram, akifichua kuwa uhusiano wake na Eric Omondi umefikia kikomo.
  • Baadhi ya wanamtandao wameonekana kutilia shaka tangazo hilo na kudokeza kuwa huenda ni kiki.

Lynne alitangaza mwisho wa mahusiano na Eric Omondi

Jioni ya Jumanne, mrembo Lynne Njihia alitoa taarifa ya kushangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram, akifichua kuwa uhusiano wake na mchekeshaji Eric Omondi umefikia kikomo.

Katika ujumbe wake wa dhati, Lynne alieleza kuwa hatua hiyo haikuwa rahisi, lakini ni bora kwa ustawi wake wa kiakili, ukuaji wake binafsi, na maisha bora anayoyatamani kwa ajili yake na binti yao.

“Nimechukua uamuzi wa kumaliza uhusiano wangu na Eric Omondi. Haikuwa rahisi, lakini ni kwa ajili ya amani yangu, ukuaji wangu, na mustakabali ninaouona kwa ajili yangu na binti yangu,” Lynne aliandika.

 “Kwa mwanzo mpya—daima,” alihitimisha.

Muda mfupi baadaye, kwenye mtandao huohuo, Lynne alipakia video ya burudani (reel) akiimba wimbo wa “Too Little Too Late” wa msanii JoJo — ambao unaelezea msichana anayemwacha mpenzi aliyemkosea, na anamkataa anapojaribu kurudi maishani mwake. Video hiyo iliibua hisia kuwa kuna zaidi ya kile kilichoandikwa.

Tangazo hilo lilikuja siku chache tu baada ya Eric kumsherehekea Lynne kwa ujumbe wa mapenzi kwenye Instagram wakati wa siku yake ya kuzaliwa, akisema: “Kheri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wa maisha yangu… mama wa mtoto wangu. Mimi na @kyla.omondi tuko hapa kukuunga mkono, mpenzi. TUNAKUPENDA sana.”

Mwezi mmoja kabla, Lynne pia alikuwa amemwandalia Eric video ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa yenye kichwa “Kheri ya kuzaliwa mpenzi wangu.”

 “Namshukuru Mungu kwa kutuweka pamoja. Mimi na Kyla ni watu wenye bahati sana duniani. Naomba maono na ndoto zako zote zitimie. Unamaanisha kila kitu kwangu, mpenzi. Napata msisimko kila ninapofikiria jinsi ninavyokupenda. Wewe ni kila kitu kwangu,” alisema.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mwezi Aprili 2020 wakati Lynne alipojitokeza kwa majaribio ya kushiriki katika moja ya vipindi vya vichekesho vya Eric. Uhusiano wao wa kikazi uligeuka kuwa wa kimapenzi baadaye.

Ingawa tofauti ya umri kati yao ni miaka 19, Lynne aliwahi kusema kwenye mahojiano kwamba msingi wa mahusiano yao ulikuwa urafiki wa kweli na kuelewana.

“Naamini kuwa mapenzi ni mapenzi. Haina kikomo, haina jinsia, haina umri. Mapenzi ni mapenzi," alisema.

Taarifa hiyo ya kuachana imezua mjadala mitandaoni. Wakati mashabiki wengi na watu maarufu walituma jumbe za faraja na matumaini, wengine walionekana kushangazwa au kuwa na maswali kuhusu kilichosababisha mwisho wa uhusiano huo.

Wengine pia walionekana kutilia shaka tangazo hilo na kudokeza kuwa huenda ni kiki.

Lakini kwa ujumbe wake, Lynne aliweka wazi kuwa amechagua utulivu, uponyaji wa ndani, na mwanzo mpya wa maisha.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved