
Msanii maarufu wa burudani mitandaoni, Remcy Don anayefahamika pia kwa jina la kisanii "Jason Derulo wa Kenya", ameonekana kujitokeza na kupinga vikali madai yanayoenea mitandaoni kuwa ndiye baba wa mtoto wa mchekeshaji maarufu Mamitto..
Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Remcy Don alieleza wazi kutofurahishwa na uvumi huo, huku akiwaomba wanablogu na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuheshimu mipaka ya maisha binafsi.
“Tafadhali, tafadhali, tafadhali... Mimi si baba wa mtoto wa mtu yeyote,” alisema Remcy Don kwa msisitizo.
Msanii huyo anayefanana sana na mwimbaji wa Marekani Jason Derulo aliongeza kuwa haelewi ni vipi watu wanafikia hitimisho kama hilo bila uthibitisho wowote:
“Mnajuaje hata baba wa mtoto ni nani? Tuache utani, tuwe wakubwa.”
Remcy Don ambaye amekuwa akionekana mara kadhaa akiigiza pamoja na Mamitto kwenye video za ucheshi, amesema kuwa urafiki wao wa kikazi usiwe sababu ya kumhusisha na mambo ya binafsi ya mchekeshaji huyo.
“Nina familia na maisha yangu binafsi ya kushughulikia. Hii tabia ya kunipachika watoto wa mtandaoni—sitaki kabisa,” alisema kwa hasira.
“Tuheshimiane jamani. Vinginevyo... usiku mwema.”
Taarifa hiyo imeibua maoni tofauti kutoka kwa mashabiki na wafuasi wake, baadhi wakimtetea huku wengine wakitaka Mamitto naye ajitokeze kutoa msimamo wake.
Hadi sasa, Mamitto hajazungumza hadharani kuhusu madai hayo, huku jamii ya mitandaoni ikiendelea kushiriki mjadala kwa hisia mseto.
Hapo awali Mamito alifichua kwamba babake mtoto si maarufu, ambayo ni moja ya sababu zilizomfanya amfiche.
Baada ya kutangaza ujauzito wake mwishoni mwa mwaka jana, Wakenya na wanamitandao wenye hamu ya kujua walihoji haraka kuhusu mpenzi wake.
Wakati huo, mchekeshaji huyo alikiri kwamba
anampenda na kuahidi uaminifu wake kwake, akisema anavutiwa naye tu