
Nyota wa muziki wa Reggae [Dancehall] wa Jamaika Chris Martin amewasili nchini Kenya jana Jumatano kwa ajili ya tamasha la Sauti Kutoka Afrika 'Sounds from Africa' linalotarajiwa kufanyika katika bustani za Uhuru, Jumamosi hii.
Msanii huyo maarufu kwenye miziki ya Raggae alifika nchini Kenya kwa mara ya kwanza mwaka 2010 na Mara ya mwisho alikua nchini mwezi Disemba 2019.
Akiwasili alielezea furaha yake ya kurejea Kenya baada ya zaidi ya miaka mitano, na kuongeza kuwa Kenya imekuwa kama nyumbani kwa upande wake.
"Nina furaha kurudi hapa tena. Nilikuja hapa kwa mara ya kwanza miaka 15 iliyopita na Wakenya hawajakuwa wakinionyesha kitu chochote zaidi ya upendo tangu wakati huo. Nina furaha kubwa kwa mashabiki wangu wa Kenya na ninafurahi kwamba, baada ya miaka yote hii, wameendelea kusimama na mimi na kuunga mkono muziki wangu," alisema Chris Martin.
Mwanamziki huyo pia alieleza kwamba anapendezwa na kufufurahishwa sana na miziki ya kenya na atajitahidi kuendelea kufanya kazi na wasani wa humu nchini.
"Nimepanda jukwaani na wasani kama vile Wyre na Willy Paul. Mimi pia ni shabiki mkubwa wa wasani kama vile Khaligraph Jones na Bien. Nasikia nyimbo nyingi za Kenya. Napenda sana wimbo wa "Extra pressure". Ina vibes nzuri sana na inanikumbusha muziki mwingi wa Jamaika." alisema.
Extra Pressure ni kazi iliyofanywa na mwanaziki Bien akimshirikisha Bensoul.
Martin ameeleza kwamba ana imani ya kuteka anga ili kuwaburudisha wafwasi wake atakapokuwa akipanda jukwaani siku ya Jumamosi Katika bustani ya Uhuru.
"Siwezi kukosa kusubiri kwa hamu siku ya Jumamosi. Ninatoa wito kwa mashabiki wangu wote, hasa wanawake wazuri wa Kenya, kujitokeza kwa mamia yao, kwa maelfu yao, na kufurahia onyesho. Haitakuwa chochote ila furaha ya kipekee na muziki mzuri," alisema.
Baadhi ya vibao vya Marti ambavyo viliwahi kifanya vizuri zaidi ni pamoja na ' weekend Love, Is it over, Paper Loving, Take my Wings miongoni mwa vingine.