logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rayvanny atanioa ila sina haraka na ndoa: Fahyvanny

Mwanamitindo Fahyvanny amefunguka na kusema kwamba hana haraka na ndoa

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako18 February 2025 - 16:20

Muhtasari


  • Akizungumza ameeleza kwamba haoni shida ya kuoleka kwa mtu maarufu kutokana na mikiki mikiki ambayo huwakumba hasa kutoka na umma kuwafatilia kwa kina na wala hawana maisha ya usiri.
  • Mahusiano ya Fahyvanny na Rayvanny yamekuweko kwa muda mrefu

Mwanamitindo Fahyvanny amefunguka na kusema kwamba hana haraka na ndoa. Ameeleza kwamba maswala ya ndoa ni mipango ya mwenyezi Mungu ila ana imani Rayvanny atamuoa.

Alikuwa akizungumza kuhusu wimbi la watu maarufu kuoa na kuolewa akirejelea harusi ya Mobeto na vilevile Diamondi ambaye ameweka wazi kwamba yuko kwenye harakati ya kufunga ndoa.

Hapana "sina presha" kuolewa ni mipango ya Mungu, kila mtu ataolewa kwa wakati wake, inshallah mbona wakati wangu wa kuoleka usifike wakati mimi ni mwanamke. nina imani na mwanaume wangu 'Rayvanny'," ameeleza Fahyvanny.

Akizungumza ameeleza kwamba haoni shida ya kuoleka kwa mtu maarufu kutokana na mikiki mikiki ambayo huwakumba hasa kutoka na umma kuwafatilia kwa kina na wala hawana maisha ya usiri.

"Mimi sioni mikiki mikiki, naona tu ni maisha ya kawaida na penzi letu liko sawa na mwanaume wangu, aliongeza.

Wakati huo ameeleza kwamba ni haki ya kila mwanadada kuishi maisha yanayompendeza na kuchagua wakati wake wa kuingia katika ndoa ila yeye hawezi kamwe kutoa ushauri kwa mtu yeyote.

"Kila mtu na mtazamo wake, kwa sasa siwezi kusema naweza kumushauri mtu, kila mtu mwenyewe na maisha yake moyo wa mtu ndio husema. kila mtu ana reality ya maisha yake, mimi siwezi kumushauri mtu kitu," alisistiza mwanamitindo huyo.

Mahusiano ya Fahyvanny na Rayvanny yamekuweko kwa muda mrefu. kuna kipindi ilisermekana wametengana baada ya miaka mitatu wakawa wanaonekana pamoja tena ila kwa upande wake Fahyvanny alisema kwamba hawajawahi kukosana.

Kwenye mahojiano na vyombo vya habari vya Tanzania, Fahyvanny alielezea mkanganyiko wake kuhusu wakati madai ya kuvunjika kwa ndoa hiyo yalitokea, akisema kuwa hana kumbukumbu ya tukio hilo.

"Kwanza, mi sijawahi kukosana na mpenzi wangu. La pili sijui mnazungumzia wakati gani. Mi sikumbuki. Labda nilikufa kidogo alafu ndio nimerudi tena," Fahyvanny alisema na kuondoa dukuduku liliokuwepo kuhusu Mahusiano yake na mwanamziki huyo wa bongo Tanzania.

Mapenzi yao yalianza kurudi sawa wakati Rayvanny alimuhusisha kwenye video yake. Wimbo huo ulitumika kama ishara ya kuweka wazi kwamba wanandoa hao walikuwa wamepatanisha na walirudi pamoja baada ya kuvunjika mnamo 2020.

Katika mashairi ya wimbo huo, Rayvanny aliahidi upendo wa milele kwa Fahyvanny na kuonyesha hamu yake ya kuwa naye kwa maisha yao yote.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved