

KIONGOZI wa chama cha ODM amefanya mkutano na wawakilishi wa wadi ambao wanatoka katika jamii ya Omogusii kutoka kaunti za Nyamira na Nairobi.
Akitoa sasisho kupitia kurasa zake za
mitandao ya kijamii, Odinga alifichua kwamba mkutano huo pia uliwahusisha baadhi
ya viongozi wa jamii ya Omogusii japo hakufichua ajenda ya mkutano huo.
Viongozi hao waliongozwa na mwakilishi
wadi ya Kilimani kaunti ya Nairobi, Moses Ogeto na wenzake Duke Masir awa wadi
ya Nyamira Township na George Morara kutoka kaunti ya Nyamira.
“Nilikutana na kundi la MCAs na
viongozi wa jamii ya Kisii kutoka Kaunti za Nyamira na Nairobi. Tulijadili
maeneo ya pamoja ya ushirikiano na maendeleo. Timu hiyo iliongozwa na George
Morara, Duke Masira na Moses Ogeto,”
Raila Odinga alifichua akiambatanisha na msururu wa picha kutoka kwa mkutano
huo.
Mkutano huo unajiri siku chache baada ya
Odinga kufokewa kwa hasira na mashabiki wa soka waliofurika katika ug awa Gusii
kushuhudia uzinduzi wa jezi mpya za klabu ya jamii hiyo, Shabana FC.
Odinga aliandamana na gavana Simba Arati
katika hafla hiyo ya Shabana FC iliyofanyika wikendi iliyopita, siku mbili tu
kabla ya kutia Saini mkataba wa kufanya kazi Pamoja kati ya ODM na UDA.
Katika kile kilichoonekana
kutowafurahisha wengi haswa kutoka jamii ya Omogusii, waliondoka kwa ghadhabu
katika uwanja huo huku wakimtupia Odinga maneno wakimuita msaliti.
Tangu kutia Saini mkataba wa kufanya kazi
Pamoja na serikali ya William Ruto, Odinga amepata wakati mgumu kuwaelewesha
wafuasi wake ambao baadhi wanahisi kwamba aliwasaliti.
Hata hivyo, kabla ya kufokewa katika
uwanja wa Gusii, Odinga alitetea muungano huo katika kaunti ya Migori ambapo
alisisitiza kwamba hajasaliti mtu yeyote.
Kwa mujibu wa Odinga, hatua ya kuungana
kwa ODM na UDA ni kwa manufaa ya wananchi wote, kauli ambayo imekuwa
ikisisitizwa na rais Ruto katika maeneo mbalimbali.
Ruto anasisitiza kwamba kuungana na
Odinga ni hatua moja katika safari ya kuleta maendeleo katika kila eneo la
taifa lakini pia kutokomeza ukabila katika siasa za Kenya.