
WAZIRI wa watoto na elimu wa Iceland amejiuzulu baada ya kukiri kuwa alikuwa na mtoto na kijana mdogo zaidi ya miongo mitatu na nusu iliyopita, kulingana na vyombo vya habari vya Iceland.
Ásthildur Lóa Thórsdóttir alifichua kwamba alianza uhusiano
na mvulana mwenye umri wa miaka 15 alipokuwa na umri wa miaka 22 na alipata na
mtoto wa kiume naye, shirika la utangazaji la Iceland la RUV liliripoti
Alhamisi iliyopita.
Thórsdóttir alikutana na mvulana huyo alipokuwa akifanya kazi
kama mshauri wa kikundi cha kidini, kabla ya kujifungua mtoto wake alipokuwa na
umri wa miaka 23 na yeye alikuwa na miaka 16.
Umri wa idhini ni miaka 15, kulingana na kanuni ya adhabu ya
nchi. Hata hivyo, ni kinyume cha sheria kwa watu wazima kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mtoto chini ya miaka 18 iwapo watapewa dhamana ya kuwafundisha,
huku wahusika wakikabiliwa na kifungo cha miaka 12 jela.
Baba aliiambia RUV hajawahi kujiona kama mwathirika katika
hali hii, lakini alibainisha kuwa alikuwa katika mahali pagumu katika maisha
yake na nyumbani aligeukia kikundi cha kanisa kwa msaada.
Kituo cha utangazaji cha umma cha Iceland kiliripoti kuwa uhusiano
huo ulikuwa wa siri lakini baba alikuwepo wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wake na
hapo awali aliruhusu mawasiliano, lakini karibu ufikiaji wote ulikatishwa kabla
ya mtoto wake kutimiza umri wa miaka 1.
Hata hivyo alitakiwa kulipa karo ya watoto kwa miaka 18.
Baba mdogo aliomba usaidizi kutoka kwa Wizara ya Sheria na
huduma ya familia ya kanisa ili kumwona mtoto wake, lakini Thórsdóttir alikataa
haki yake ya kutembelewa, kulingana na shirika la habari la umma la Iceland.
Muda mfupi baada ya ripoti ya RUV siku ya Alhamisi,
Thórsdóttir alijiuzulu kutoka nafasi yake ya uwaziri, shirika la utangazaji la
umma lilisema. Ataendelea kuwakilisha Chama cha Wananchi kama mbunge.
Waziri mkuu wa Iceland alisema Thórsdóttir alikutana na
viongozi watatu wa chama lakini ulikuwa uamuzi wake kujiuzulu, kulingana na
RUV.
"Tulijadili chaguzi pamoja na kusikia maelezo yake ya
suala hilo kwa undani kwa mara ya kwanza kwenye mkutano huo," Waziri Mkuu
Kristrún Frostadóttir alisema katika mkutano wa wanahabari Ijumaa, RUV
iliripoti. Kiongozi huyo alikariri kwamba Thórsdóttir alikuwa amechukua jukumu
haraka kwa kujiuzulu.
"Kwa kweli, hili ni jambo la kusikitisha, lakini
halihusiani na kazi yetu," Frostadóttir alisema, akiongeza kuwa ofisi ya
waziri mkuu ilikuwa haijamaliza kuchunguza suala hilo tangu ilipoletwa kwao
wiki moja iliyopita.