

Shirika la habari la RFI Kiswahili liliripoti kuwa watatu hao walikuwa miongoni mwa watu 37 ambao walihukumimiwa kifo mwezi Septemba mwaka jana [2024] na mahakama ya kijeshi.
Watatu hao walituhumiwa kwa kuongoza mashambulio katika ikulu ya rais na nyumba ya mshirika wa rais Felix Tseshekedi mwezi Mei mwaka jana.
Kutupiliwa mbali kwa hukumu hiyo kunajiri kuelelea ziara ya mshauri mkuu wa rais wa Marekani kuhusu mambo ya Afrika Massad Boulos.
Mshauri huyo ambaye ni mtu wa karibu sana na familia ya rais Trump anatarajiwa kuwasili nchini DRC siku ya leo Alihamisi.
Mshauri huyo wa rais wa marekeni pia anatarajiwa kuzuru hapa nchini Kenya, taifa jirani la Uganda na vilevile Rwanda.
Wizara ya mambo ya nje ya kimarekani ilibaini kwamba awali kulikuwepo na mazungumzo kuhusu hilo swala la kuhukumiwa kifo kwa raia wake nchini DRC. Raia hao walipatikana na hatia ya njama ya uhalifu, ugaidi miongoni mwa mengine ambayo waliyakanusha.
Mshukiwa mkuu wa jaribio hilo ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Congo aliuwawa wakati wa shambulio hilo pamoja na wengine watano.
Kwa jumula watu 51 walihukumiwa na mahakama ya kijeshi wakati wa kuamua kesi hiyo ambayo ilipeperushwa kwenye vyombo vya habari vya nchi ya DRC.
Hukumu za vifo hazijatekelezwa nchini Demokrasia ya Congo kwa takribani miaka 20 na badala yake wafungwa wanaopokea adhabu hio hutumikia kifungo cha maisha jela.
Serikali yaq nchi hiyo iliondoa sheria ya kutowanyonga wahalifu mwezi machi mwaka huu ikitaja haja ya kuwaondoa wasaliti wa jeshi la taifa lakini hakuna hukumu ya kifo iliyotekelezwa tangu wakati huo.
Haijabainika iwapo raia wengine wa Uingereza, Ubeligiji na Canada pia watabadilishiwa vifungo vyao.