
Mwanahabari Moses Dola Otieno ameachiliwa huru baada ya Jaji wa Mahakama ya Juu Alexander Muteti kukubali ombi lake la kutathmnii upya hukumu yake.
Mahakama hiyo pia iliagiza idara ya magereza kumwachilia mara moja isipokuwa azuiliwe kwa kosa lingine.
Uamuzi huo ulitolewa kwa njia video, ambapo Dola alitoa shukrani kwa hakimu na kushiriki matumaini yake ya kufika mbele yake tena baada ya kumaliza mafunzo yake ya uanasheria.
Dola, alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 10 kwa mauaji ya mkewe, Sarah Wambui Kabiru, 2011, mwanahabari mwenzake.
Alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mwaka wa 2018 baada ya mahakama kupata kwamba Wambui alifariki kufuatia ugomvi wa nyumbani kwao jijini Nairobi. Dola baadaye alijisalimisha kwa mamlaka baada ya kujificha.
Akiwa gerezani Dola ajiunga na kozi ya uanasheria, na tayari amejisajili kwa cha Sheria nchini (KSL).