logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Natazamia kushirikiana nawe!" Rais Samia ampa pongezi za dhati Youssouf baada ya kushinda uchaguzi wa AUC

Youssouf alishinda uchaguzi wa mwenyekiti wa AUC baada ya kupata kura zinazohitajika katika raundi ya saba.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri16 February 2025 - 09:26

Muhtasari


  • Rais Samia alieleza matumaini yake ya kushirikiana na Youssouf katika juhudi za pamoja za kufanikisha Afrika yenye ustawi, umoja, na amani. 
  • Rais William Ruto pia alimpongeza Youssouf kwa ushindi wake na akamhakikishia kwamba Kenya itashirikiana naye.

Rais Samia Suluhu amempongeza Mahamoud Youssouf

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amempongeza kwa dhati Waziri wa mausala ya kigeni wa zamani wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf kwa kuchaguliwa kwake kama Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

 Katika ujumbe wake za pongezi, Rais Samia alieleza matumaini yake ya kushirikiana na Youssouf katika juhudi za pamoja za kufanikisha Afrika yenye ustawi, umoja, na amani. 

"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Mahamoud Ali Youssouf kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Natarajia kushirikiana nawe katika harakati zetu za pamoja za kufikia Afrika iliyo na ustawi zaidi, iliyoungana na yenye amani," alisema Rais Samia. 

Katika uchaguzi huo, Youssouf alishinda baada ya kupata kura zinazohitajika katika raundi ya saba, ambapo alikuwa mgombea pekee baada ya mgombea wa Kenya RailaOdinga kuondolewa katika raundi ya sita. 

Richard Randriamandrato wa Madagascar aliondolewa mapema baada ya kushika mkia katika awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne na kuwaacha Raila na Youssof kumenyana.

 Youssouf alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 33 zilizohitajika katika raundi ya saba ya upigaji kura, ambayo alishinda peke yake.

 Baada ya uchaguzi huo, mgombea wa Kenya Raila Odinga, alikubali matokeo na kusema kuwa demokrasia ilizingatiwa kikamilifu na akampongeza mshindi.

 “Ninakubali matokeo ya kura. Kwa hivyo, ninakubali kushindwa,” alisema Raila, akisisitiza kuwa uchaguzi huo ni mfano wa kuimarisha demokrasia barani Afrika.

 Alieleza kuwa alikuwa tayari kwa matokeo yoyote na kwamba hana kinyongo na uamuzi wa wakuu wa mataifa ya Umoja wa Afrika..

 Kiongozi huyo wa ODM aliongeza kuwa alitimiza wajibu wake kama mgombea kwa kukutana na viongozi mbalimbali wa Afrika na kushiriki maono yake kwa AUC.

 Katika hotuba yake, Raila alitoa shukrani kwa wale waliompigia kura pamoja na wale waliompigia mpinzani wake, akisema wote walitekeleza haki yao ya kidemokrasia.

 “Ninawashukuru wale waliopiga kura kwa kunichagua. Pia nawapongeza waliompigia mwenzangu kwa kuwa walitumia haki yao ya kidemokrasia,” alisema.

 Raila alimtakia kila la herimshindi, Mahamoud Ali Youssouf wa Djibouti, akimpongeza kwa kupata ridhaa ya viongozi wa Afrika kuongoza Umoja wa Afrika.

 “Namtakia mpinzani wangu kila la heri. Namtakia mafanikio katika majukumu yake mapya,” alisema.

Rais William Ruto pia alimpongeza Youssouf kwa ushindi wake na akamhakikishia kwamba Kenya itashirikiana naye anapoongoza Tume ya Umoja wa Afrika.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved