
Matamshi ya aliyekuwa Naibu wa Rais Bwana Rigathi Gachagua ya kumtetea jaji mkuu Martha Koome yaliibua tetesi nyingi miongoni mwa viongozi.
Siku ya Jumapili ya tarehe 23,2025 Rigathi Gachagua akiwa Kaunti ya Meru katika hafla ya umma aliweza kutoa madai kuwa anafahamu njama iliokuwa ikipangwa na serikali ili kumuondoa Jaji mkuu Maatha Koome afisini.
Kwa kujibu kauli hiyo ya Gachagua naibu wa Rais Kithure
Kindiki katika chapisho kwenye mtandao wake wa X aliweza kusema kuwa suala la
kupata nafasi kama jaji mkuu au kuondolewa si jambo la siasa bali ni jambo la
kikatiba na ambalo hufuta taratibu za Katiba na Sheria.
Seneta wa Makueni Dan Maanzo katika usemi wake alipohojiwa
na kituo kimoja cha runinga nchini aliweka mambo paruwanja kwa kusema kuwa hilo
jambo la kutaka kumuondoa jaji mkuu Martha Koome si jambo la siri ila ni jambo
ambalo linajulikana.
Alifafanua akisema kuwa
si mara moja au mbili aliwahi kuraiwa na viongozi wa kutoka mrengo wa Kenya
Kwanza wakihitaji huduma zake ili kuasisi mchakato huo wa kuwang’atua majaji
afisini.
Alielezea kwa kusema kuwa hilo ni jambo ambalo huchukua
mkondo wa siasa kwa hivyo ikiwa ulichaguliwa kutokana na nguvu za kisiasa bila
shaka kuwa tayari kundolewa kisiasa
,alieleza kuwa mara nyingi mambo hayo huchukua mkondo wa siasa.
Kwa upande wake Seneta Richard Onyonka naye alisema kuwa matamshi ya bwana Gachagua ya kusema kuwa iwapo rais Ruto ataitikia Martha Koome kuondolewa asikanyage Meru ni tamko la kuleta chuki na uhasama akisema kuwa kwa Bahati mbaya jambo baya limtendekee rais akiwa huko itakuwa vipi au itasemekana vipi.
Kwa upande mwingine mbunge wa Kimilili Mheshimiwa Didimus
Barasa katika ukurasa wake wa X aliweza kutilia doa hali ya Jaji Koome kusalia
kimya huku Rigathi Gachagua akiwa ndiye
anayemtetea ni nani kwa nini atetewe ilihali jaja anafahamu kazi yake ambayo
imo katika misingi ya Katiba?
Kwa upande mwingine mheshimiwa Gakuya alinukuliwa akimtetea Gachagua kwa kusema kuwa wabunge kutoka jamii ya Mulembe bungeni kuna mbunge aliyetetea spika Wetang’ula kutoguswa kwa vyovyote vile ilihali Gachagua akitetea wa kwao wanamsuta eti ni mkabila.
Hata hivyo jambo la kuondoa jaji mkuu au kusalia afisini ni jambo la kisheria ambalo linaipa
tume ya JSC kutekeleza wajibu huo pasi na kuingiliwa na wanasiasa au watu wenye
nia ya kusambaratisha haki na uhuru wa mahakama.