
Rais William Ruto na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga wameingia rasmi katika makubaliano ya kisiasa yatakayoshuhudia vyama vyao vikishirikiana.
Mkataba wa Ushirikiano kati ya Kenya Kwanza na ODM ulisainiwa Ijumaa katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, kwenye hafla iliyohudhuriwa na Wabunge wanaomuunga mkono kila kiongozi.
Naibu Rais Kithure Kindiki pia alihudhuria hafla hiyo.
Kupitia mkataba huu, vyama vya UDA na ODM vitashirikiana katika masuala ya kitaifa kwa kutumia miundombinu yao ya kisiasa.
Pia, vyama hivyo vitawatumia wataalamu wao mahiri kwa mashauriano kuhusu utawala na sera za kitaifa.
Kabla ya hafla ya utiaji saini, maelfu ya wafuasi wa ODM walikusanyika katika KICC kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Hafla hiyo ilifuatia mfululizo wa mashauriano ambayo kiongozi
wa ODM Raila Odinga alifanya katika maeneo mbalimbali nchini ambako ana uungwaji
mkono mkubwa wa kisiasa.