

Serikali ilianzisha mpango wa kutoa michango kwa wanabodaboda na akina mama eneobunge la Kiambaa
Ni shuguhuli iliyofanyika katika shule ya upili ya Karuri eneobunge la Kiamba kaunti ya Kiambu.
Ni hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi wakuu serikalini wakiongozwa na Naibu wa rais Profesa Abraham Kithure Kindiki, kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichungw'ah, mbunge wa Kapseret Oscar Sudi miongoni mwa viongozi wengine.
Katika hafla hiyo ambayo ilikuwa na mbwembwe pamoja na wananchi waliofurika kuweza kuhudhuria shughuli hiyo viongozi mbalimbali waliweza kutoa hotuba zao kuweza kuisifia serikali na kuwarai wananchi waweze kuiunga mkono serikali kikamilifu.
Reuben Kiborek mbunge wa Mogotio aliweza kusema kuwa wananchi walistahiki kuwa watulivu huku serikali ikihakikisha kuwa inatimiza kila ahadi iliyoahidi ilipoingia mamlakani.
''Viongozi wengi wamekuwepo katika uongozi wa taifa wakati ambapo kulikuwa na viongozi wengine wakawa wanakumbana na chngamoto mlisema kuwa tuipe serikali muda ili iweze kutekeleza ahadi zake na wakati ambapo kiongozi wetu amechukua mamlaka watu wanaanza kusema ni lazima aende aaaah je hiyo ni haki kweli?''Mbunge Reuben Kiborek alisema.
Kwa upande mwingine Mbunge wa Kapsaret Sudi aliweza kusema kuwa haiwezekani kutafuta au kufanya kazi kwa bidii ili kupata jambo kisha baadaye uwachiliee tena urudi katika viwango vya kuanza kutafuta tena kwa kwanza kwa hatua moja.
'' Haiwezekani kwa mtu kuweza kutafuta jambo kwa muda mrefu kisha ukishapata unaachilia tena uanze kutafuta upya ni kama tu utafute chakula kwa kusumbukana kisha ukipata mlo tena unapiga teke unarudi tena kuanza kutafuta la hasha ha iwezekani.'' Oscar Sudi alisema.
kwa upande wake Naibu wa Rais Kithure Kindiki aliweza kusema kuwa kama tu viongozi waliotangulia na kufanikisha maendeleo ya kuisukuma nchi mbele na kuendelea kupiga hatua aliwahakikishia wakazi wa Eneobunge la Kiambaa kuwa nao walikuwa katika harakati ya kuhakikisha kuwa taifa linasonga mbele kimaendeleo.
Tangu serikali ya Kenya Kwanza ilipochukua hatamu za uongozi hio ndio hafla ya kwanza ya kuweza kuandaliwa ambapo ilikuwa ikipigia debe mfumo wa kuhakikisha kuwa inapata kumuinua mtu wa kiwango cha chini.
Katika hafla hiyo Kindiki alitoa mchango wa shilingi milioni tatu kwa niaba ya rais huku yeye akitoa milioni mbili vilevile mbunge Oscar Sudi alitioa kitita cha shilingi milioni mbili, Kimani ichungwa akitoa mchango wa shilingi milioni moja ilihali wabunge wengine wakitoa michngo ya shilingoi laki moja .