logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu wachezaji wakubwa Ulaya ambao bado wapo huru kujiunga na vilabu vingine

Isco anapakia mikoba yake Bernabeu msimu huu

image
na Davis Ojiambo

Michezo23 June 2022 - 13:33

Muhtasari


  • •Baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa barani Ulaya wapo  kama wachezaji huru msimu huu wa joto huku kandarasi zao kwenye vilabu vyao vya sasa zikimalizika.
  • •BBC Sport inaangazia kwa karibu uteuzi wa majina yanaojiandaa kupata waajiri wapya kwa msimu ujao.
Ligi ya soka ya Uingereza

Baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa barani Ulaya wapo  kama wachezaji huru msimu huu wa joto huku kandarasi zao kwenye vilabu vyao vya sasa zikimalizika.

Je, Paul Pogba atarejea Juventus? Je maisha yatakuwaje baada ya Real Madrid kwa Gareth Bale? Na Christian Eriksen anaweza kuishia wapi baadaye?

BBC Sport inaangazia kwa karibu uteuzi wa majina yanaojiandaa kupata waajiri wapya kwa msimu ujao.

Gareth Bale

Klabu ya sasa: Real Madrid

Anahusishwa na: DC United, Cardiff City, Newcastle United, Nottingham Forest, AC Milan, Tottenham Hotspur.

Kuondoka kwa Gareth Bale kutoka Real Madrid kunakuja baada ya kubeba kombe kwa miaka tisa, ambapo alishinda mataji matano ya Ligi ya Mabingwa na La Liga mara tatu.

Mshambuliaji huyo wa Wales, 32, alijiunga na mabingwa hao wa Uhispania Septemba 2013 kwa dau la uhamisho lililoweka rekodi ya dunia kwa wakati huo ya zaidi ya £80m.

Tayari ameeleza kuwa familia yake na kujiimarisha kwa ajili ya Kombe la Dunia vitakuwa vipaumbele vyake vikuu atakapoamua pa kucheza msimu ujao.

Paul Pogba

Klabu ya sasa: Manchester United

Anahusishwa na: Juventus, Real Madrid, Paris St-Germain, Manchester City.

Paul Pogba anaondoka Manchester United msimu huu wa joto baada ya kufanya vibaya kwa miaka sita katika kipindi chake cha pili katika klabu hiyo.

Kiungo huyo alishinda Kombe la EFL na Ligi ya Europa ndani ya mwaka mmoja baada ya kurejea kwa kishindo sana United katika uhamisho ulioweka rekodi ya dunia ya wakati huo wa £89m kutoka Juventus mwaka 2016.

Ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliisaidia Ufaransa kushinda Kombe la Dunia mwaka wa 2018, ameonesha tu uchezaji wake bora wa pasi na fowadi mwenye nguvu United, ambapo mara nyingi amekuwa akiwajibika katika safu ya ulinzi na kuwakasirisha mashabiki kwa kushindwa kuonesha juhudi.

Katika makala iliyoangazia maisha yake binafsi, Pogba aliripotiwa kuwa madai ya ofa ya mkataba wa United ulioboreshwa wa pauni 300,00 kwa wiki kuwa si "chochote" akiashiria kwamba yeyote atakayemsajili atahitaji kuwa na mifuko mirefu zaidi.


Christian Eriksen

Klabu ya sasa: Brentford

Anahusishwa na: Brentford, Tottenham, Manchester United

Christian Eriksen anafaa kuwa sehemu ya kandarasi ya miaka minne na nusu katika klabu ya Inter Milan.

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alipatwa na mshtuko wa moyo wakati akicheza Euro 2020 mwezi Juni mwaka jana nchini Denmark na kubadilisha maisha yake ya soka na kurejea kwenye soka baada ya kuwekewa kifaa kwenye moyo  Implantable Cardioverter Defibrillator (ICD).

Hilo lilimfanya Eriksen kuachiliwa na Inter - kwa sababu kifaa cha ICD hakiruhusiwi katika Serie A - na hivyo kwenda Brentford kwa mkataba wa miezi sita ambapo ubora wake uling'aa alipoisaidia timu kupata hadhi ya Ligi Kuu.

The Bees wana nia ya kumbakisha mchezaji huyo wa zamani wa Ajax lakini je, atasalia London au kuelekea kwingineko pamoja na Manchester United wanaomtaka?

Jesse Lingard

Klabu ya sasa: Manchester United

Anahusishwa na: West Ham United, Newcastle, Tottenham, Roma, AC Milan

Jesse Lingard anaondoka Manchester United baada ya kukaa kwa miongo miwili na kilabu.

Wakati  United ikifanya uchaguzi huo wa kushangaza wa kumbakiza kiungo huyo wa kati wa England msimu uliopita wa joto, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alistahimili kampeni ngumu ya 2021-22 na alitumika kwa kiasi.

Kabla ya hapo uhamisho wa mkopo kwenda West Ham mapema 2021 ulitumika kama ukumbusho wa sifa zake na kutafuta klabu mpya ambayo itampa uhakika wa kucheza katika mwaka wa Kombe la Dunia inaweza kuingia kwenye mawazo yake.

Ousmane Dembele

Katika siku yake Ousmane Dembele ni mmoja wa washambuliaji wa kufurahisha zaidi katika kandanda ya dunia

Klabu ya sasa: Barcelona

Anahusishwa na: Chelsea, PSG

Mambo hayajaenda sawa kwa Ousmane Dembele tangu ajiunge na Barcelona katika moja ya mikataba ya bei ghali zaidi wakati wote kutoka Borussia Dortmund mwaka 2017.

Akiwa bado na umri wa miaka 25 tu, majeraha yametatiza maendeleo ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa, ikimaanisha kuwa ameonesha mambo machache tu kuhusu uwezo wake. Kasi yake, mbinu na uwezo wa kukimbia safu za ulinzi za wapinzani zinaweza kuwafanya mashabiki wa Nou Camp kusimama.

Ingawa mara kadhaa amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka, rais wa klabu Joan Laporta na kocha mkuu Xaxi wote wana matumaini kwamba anaweza kushawishiwa kubaki.

Edinson Cavani

Klabu ya sasa: Manchester United

Anahusishwa na: Real Madrid, Arsenal, Atletico Madrid na Juventus.

Edinson Cavani alifurahia miaka miwili akiwa Manchester United.

Fowadi huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 35, ambaye aliwasili kwa uhamisho wa bure kutoka PSG Oktoba 2020, alianza vyema akiwa na mabao 17 kwenye mashindano yote katika msimu wake wa kwanza.

Wakati wa ujio wa Cristiano Ronaldo na orodha inayoonekana kutokuwa na mwisho ya majeruhi ilimfanya apate shida msimu uliopita. Haiba yake na uzoefu bado vinaweza kuthibitisha kuwa bidhaa muhimu kwa klabu tarajiwa.

Fernandinho

Fernandinho alijiunga na Manchester City kutoka Shakhtar Donetsk kwa £34m mwaka 2013

Klabu ya sasa: Manchester City

Anahusishwa na: Botafogo, Flamengo , Corinthians, Athletico Paranaense

Fernandinho, 37, alicheza mechi 19 za Ligi ya Primia alipoisaidia Manchester City kutwaa taji lao la nne katika misimu mitano.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil tayari ameonesha nia ya kutaka kurejea katika nchi yake atakapoondoka City, ambako alishinda mataji matano ya ligi kuu, sita ya Kombe la EFL na Kombe la FA.

Luis Suarez

Anahusishwa na: Juventus, Aston Villa, Sevilla, Inter Miami

Akiwa na umri wa miaka 35, Luis Suarez ni mchezaji mwingine anayefaa katika kitengo cha wakongwe, huku akikaribia kuondoka Wanda Metropolitano akitokea msimu wa nyuma ambapo alifunga mabao 13 katika mashindano yote.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay anaweza asiwe mahiri kama alivyokuwa katika ujana wake lakini uchezaji wake na harakati zake kuelekea lengo zinaweza kushawishi vilabu kadhaa kumpa ofa ya muda mfupi.

Isco

Klabu ya sasa: Real Madrid

Anahusishwa na: Sevilla, Arsenal, Tottenham

Isco anapakia mikoba yake Bernabeu msimu huu wa joto kama mshindi mara tano wa Ligi ya Mabingwa na bingwa mara tatu wa La Liga.

Akiwa bado katika kiwango cha juu cha maisha yake ya soka, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 atajaribu kugundua tena uwezo wake baada ya kuonenaka kuwa si mchezaji pendwa kwa Madrid na kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha Uhispania.

Angel di Maria



Klabu ya sasa: PSG

Anahusishwa na: Juventus, Barcelona.

Mshambuliaji wa Argentina Angel di Maria alifurahia kadi nyekundu kutoka kwa PSG, akifunga bao katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Metz katika mchezo wake wa mwisho na hivyo kutolewa nje kwa shangwe na umati wa Parc des Princes.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alifunga mabao 93 katika mechi 295 alizochezea PSG, akishinda mataji matano ya ligi na vikombe tisa vya nyumbani wakati alipokuwa Paris,Ufaransa

Juventus na Barcelona wanadaiwa kuwania saini ya winga huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved