
Mkufunzi mkuu wa timu ya Liverpool Arne Slot amazungumzia suala la mshambuliaji wa kulia wa klabu hiyo Mouhamed Salah kutua ushindi wa Ballon d'Or...
Slot akizungumza na wanahabari amesema kwamba ni vyema kuwa Salah anajadiliwa kwa ushindi huo kwani inaashiria kwamba anafanya kazi nzuri kibinafsi na pia kwa timu nzima.
Akizungumza pia ameeleza kwamba kushinda tuzo hiyo haihitaji tu kukufunga mabao lakini pia kunyakuwa mataji. Amesisitiza kwamba wao kama timu wanafaa kushinda mataji ili kumpa Salah nafasi nzuri ya kutwaa tuzo hiyo.
"Ni jambo jema kwamba Mo yupo kwenye mjadala kwa sababu ina maana anafanya vizuri na ina maana tunafanya vizuri. Lakini ili abaki katika mjadala huo, anapaswa kuleta maonyesho sawa na alivyofanya kwa miezi saba au nane sasa.
Nadhani kwa ujumla, mtu anayeshinda Ballon d'Or anahitaji kushinda kitu pia, kwa hivyo ni changamoto kubwa mbele yetu lakini pia mbele yake," alisema kocha huyo.
"Ninachopenda sana ni kwamba anachukua changamoto hii - sio tu kwa kufunga bao kubwa na kusaidia sana dhidi ya City lakini pia alitaka timu ishinde kwa sababu kiwango chake cha ulinzi, haswa katika kipindi cha pili, kilikuwa bora. Nadhani hicho ndicho kinachohitajika kwetu kuwa na nafasi ya kushinda kitu na kama sisi kama timu tunaweza kushinda kitu, atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda tuzo ya mtu binafsi kama Ballon d'Or...," aliendelea
Kocha huyo mzaliwa wa taifa la Uholanzi ameeleza kwamba hana fikra kwamba mshindi wa Tuzo ya Ballon d'Or anafaa kubeba mataji mengi zaidi, amelinganisha na mshindi wa mwisho na kusema kwamba yeye alibeba ligii kuu pekee yake wala sio ligii ya mabingwa.
"Itaongeza nafasi yake kuwa kubwa zaidi lakini ya mwisho aliyeshinda, nadhani alishinda ligi tu na sio Ligi ya Mabingwa. Sio tu kuhusu kiasi cha mataji unayoshinda lakini nadhani hata yule aliyeshinda siku za nyuma labda - sina uhakika wa asilimia 100 - alishinda ligi au Ligi ya Mabingwa. Lakini katika soka ni kama hivi: unahitaji timu kushinda tuzo ya mtu binafsi, na hicho ndicho ambacho Mo anaelewa kwa sasa ni vizuri sana kwa sababu kiwango chake cha kazi, hasa katika kipindi cha pili lakini karibu wakati wa mchezo mzima, kilikuwa kizuri sana na chenye manufaa sana kwetu kupata nafasi ya kushinda mchezo dhidi ya City," alieleza Slot