
Mwanadada Maria Maarufu kama Malaika Cute amefunguka kwamba hawezi kuwa mwigizaji wa video "video vixen" kwenye nyimbo za wasanii.
Kulingana na mwanadada huyo chanzo kikubwa cha yeye kukataa kuwa video vixen ni kwamba wasanii wengii wanamtongoza sana.
Mwanadada huyo aliulizwa hili kutokana na u'vixen aliyofanya na mwanamziki wa bongo Harmonize. Kwa upande wake alisema kwamba kuhusika kwenye wimbo wa Harmonize kama video vixen ni kutokana na urafiki wao.
"Hapana mimi sio video vixen, hamufai kunitambua hivyo, kwenye video ya Harmonize nilifanya tu kutokana na urafiki wetu," alifichua.
Alifunguka kwamba jambo lingine ni kwamba Harmonize pia aliwahi kumsaidi wakati mmoja na sasa ilikuwa zamu yake kurejesha mkono," alisema Malaika Cute.
Pia aliongeza kwamba kilichomchochea sana kufanya kazi na Harmonize ni kwamba pia aliwahi kumsaidia wakati mwingine.
"Nilifanya kwa Harmonize kwa sababu ya urafiki wetu, na alisimama na mimi kipindi ambacho watu walijaribu kuni attack sana na nikaona ni mtu ambaye ana upendo, so nilifanya hivo," alieleza.
"Harmonize mwenyewe akaanza kuongelea hilo jambo kabla ya yeye na mimi kukutana. urafiki wetu ulianza baada ya yeye kunidefend kwenye mitandao ya kijamii," aliendelea.
Mtoto wa kike pia amefichua kwamba anatafutwa sana na wasnii mpaka wa nje ya Tanzania lakini amedinda kufanya nao kazi.
"Napochiwa sana na wasanii wakubwa nje, lakini sijakubali kufanya, nilikuwa napigiwa simu kabla ya hata Harmonize," Cute aliweka wazi.
Mrembo huyo alizaliwa katika jiji la Dar es Salaam, miakia 35 iliyopita nchiniTanzania, Malaika Cute sio sura nzuri tu bali pia ni mbunifu wa mitindo mwenye talanta ambaye amejitengenezea jina.
Cute alianzisha kazi yake ya uanamitindo akiwa na umri mdogo, lakini alipata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake la kupendeza.
Malaika Cute awali alipata umaarufu kama mwanamitindo mnamo 2021, wakati mwili wake wa kupendeza ulivutia wengi katika hafla licha ya ukweli kwamba hakuwa anashindana katika kurasa za urembo.
Malaika pia ana kampuni ya mitindo ya mtandaoni inayoitwa Malaika Fashion Design, ambayo ina utaalam katika kutoa mavazi ya kifahari, mifuko, slippers, na zaidi.