
MSANII Kevin Kioko maarufu kama Bahati amewashauri wanaume wasio na pesa kuepuka kabisa suala la mapenzi.
Akichukua kwenye ukurasa wake wa Instagram alikofichua zawadi
nambari 6 kati ya nane ambazo alianza kumpa mkewe wiki iliyopita kama njia moja
ya kusherehekea miaka 8 ya ndoa yao, Bahati alisema kwamba mapenzi na
kuchumbiana si vitu vya watu wasio na pesa.
Kwa mujibu wa msanii huyo, mwanamume yeyote anayetaka kupenda
na kupendwa sharti awe tayari kumtumia pesa zake kumfurahisha na kumpendezesha
mwanamke wake.
Alisema kwamba yeyote asiyetaka kumtumia pesa zake kwa
mwanamke, au mwenye hana pesa basi mapenzi hayamfai, na aghalabu hao ndio
huwakosea warembo heshima kwa kuwaita ‘gold diggers’.
‘Wapendwa Wanaume;
Ushauri wa heshima 🙏 Kama huna Pesa
Usichumbie 🫣 Ndio Njia Pekee Utakayoacha Kuwaita Wanawake Wachimba
Dhahabu 😎 Kwenye Post Yangu
Inayofuata Nitakuonyesha ni kiasi gani nilichotumia kwa Zawadi ya Mke Wangu
NO.6 Vito vya Wapendanao,” Bahati alisema.
Kwa takribani wiki mbili, msanii huyo amekuwa gumzo la
mitandaoni kutokana na haiba za zawadi ambazo amekuwa akimkabidhi mke wake,
Diana Marua.
Bahati alianza kumpa mkewe zawadi kama vile mashamba, mradi
wa ujenzi wa nyumba za kuishi miongoni mwa zawadi zingine kusherehekea miaka 8
ya uhusiano.
Wiki iliyopita, Bahati alijitoa kimasomaso kuchorwa tattoo ya
jina la ‘Diana B’ kwenye mkono wake kabla ya kumpa Diana Marua zawadi zingine.