
KIJANA mkwasi mwenye pesa zake kutoka Tanzania, Godlove Mwakibete maarufu kama Chief Godlove amempa msanii wa Kenya Stevo Simple Boy kitita cha hela ndefu kama zawadi.
Katika video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram,
Godlove alimkaribisha Stevo Simple Tanzania kwa Burunguti la hela noti za
Tanzania na kumwambia kwamba hizo zitakuwa za matumizi yake wakati wa kipindi
chake nchini humo.
Kisha alichomoa Burunguti lingine na kumkabidhi akimwambia
kwamba hizo zitawekwa pembeni hadi pale Simple Boy atakapotoa ngoma 3 nzuri.
Mwakibete aliahidi kwamba yeye ndiye atakayegharamia video za
ngoma hizo 3 na kumtaka Simple Boy kuchakarika na kuhakikisha ni ngoma zenye
mvuto na mnato.
“Umekaribishwa Tanzania
Stevo Simple Boy. Mimi sasa umefika kwangu na nataka ujue ukionana na Chief jua
umeonana na pesa. Wakenya wanasema thamani ya hela za Tanzania iko chini kuliko
za Kenya lakini hizi nakupa hapa ni za thamani kubwa ajabu,” Godlove alisema huku
akifungua mkoba wake wa noti.
“Hizi zote ni kwa ajili
ya matumizi yako ukiwa hapa Tanzania,” Godlove alimwambia huku
akimkabidhi hela. “Hizi hapa zingine nitakuongeza pale ambapo utatoa hitsongs 3. Hizo ngoma
3 ni mimi nitagharamia video yazo. Nakulipia mimi mtoto mdogo mwenye hela
nyingi. Na kuanzia leo wewe ni familia yangu,” Godlvoe aliongeza.
Stevo alisema hatolaza damu na atahakikisha ametoa ngoma hizo
3 ili kupata pesa hizo.
Kwa upande wake Godlove, Alifichua kiasi cha hela hizo kwa
jumla na kusema kwamba ndio rasmi amemtambulisha Stevo kwa nguvu ya pesa.
“Wakenya wananipenda sana
na Mimi narejesha baraka Zangu kwa kumbless kijana wao @stevosimpleboy8 million
40 za Tanzania 🇹🇿 kenya Ksh 1940000
nimemuunganisha na nguvu ya pesa na jicho la tatu,” Godlove alikariri.