
MSANII kutoka Kibera, Stevo Simple Boy amefichua kwamba yeye yuko tayari kufanya chochote ambacho mashabiki wake watataka afanye, mradi tu awaburudishe.
Msanii huyo alikuwa akijibu swali la iwapo yeye ni
mtengenezaji maudhui ya mitandaoni au ni mwanamuziki.
Simple Boy, ambaye anajulikana kwa mtindo wake wa rap na pia
katika siku za hivi karibuni kwa kutengeneza maudhui kupitia Kauli na semi zake
za ucheshi pamoja na uvaaji wake, alisema kwamba yuko tayari kufanya jinsi
mashabiki watakavyotaka.
Hata hivyo, alisisitiza kwamba yeye hujihisi vizuri kufanya
muziki ikilinganishwa na utengenezaji maudhui ya kuchekesha.
“Mwaka huu nimewapangia
mashabiki muziki kibao, content na vitu vingine vingi. Mashabiki ndio wanasema
kwamba mimi niko bora kwa content kuliko kwa muziki lakini mimi najua kwa
muziki niko bora,’ Stevo alisema.
“Mimi nafanya chenye
mashabiki wanataka, wakisema content niko bora kuliko muziki ni poa lakini mimi
kwangu nahisi muziki ndio niko bora,’ Simple aliongeza.
Kuhusu suala la mapenzi, Simple Boy aliradidi kwamba kwa sasa
yuko singo huku akisema kwamba mtoto aliyezaliwa na mpenzi wake wa awali si
wake.
Alisema kwamba kwa sasa hafikirii kama atajitosa kwenye
ulingo wa mapenzi tena, akidokeza kwamba mpenzi wake wa zamani alimsaliti.
“Mtoto si wangu, kwa sasa
niko single na sitaki mahusiano ya mapenzi kwa sasa. Mimi niko sawa na mambo ya
mapenzi nimeachana nayo kabisa kwa hiyo mashabiki zangu msitarajie shemeji yenu
hivi karibuni,” alisema.
Kuhusu kurudiana na mpenzi wa kwanza, Pritty Vishy, Stevo
alisisitiza kwamba hakuna jinsi watarudiana akitumia msmo maarufu kwamba ‘huwezi
ukayarudia matapishi’.