logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Staa wa Reggea Don Campbell Atua Kenya Kabla ya Tamasha la Wikendi

Mwimbaji maarufu wa reggae kutoka Uingereza Don Campbell yuko nchini Kenya.

image
na Samuel Mainajournalist

Mastaa wako12 February 2025 - 07:37

Muhtasari


  • Campbell aliwasili katika Uwanja wa JKIA siku ya Jumanne asubuhi, kabla ya tamasha lake lililotarajiwa wikendi ijayo.
  • Don Campbell pia aliweka wazi kuwa anatazamia kukutana na mashabiki wake wa Kenya.
Don Campbell ametua nchini Kenya

Mwimbaji maarufu wa reggae kutoka Uingereza Don Campbell yuko nchini Kenya.

Mwimbaji huyo mahiri wa reggae aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta siku ya Jumanne asubuhi, kabla ya tamasha lake lililotarajiwa wikendi ijayo.

Campbell anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la hisani kwa jina ‘Reggea With A Cause’ ambalo litafanyika katika ukumbi wa KICC Jumamosi, Februari 15. Hii kitakuwa shoo ya pili kwa msanii huyo wa reggae kutumbuiza katika bara la Afrika.

"Ni furaha kuwa hapa. Ni furaha zaidi kuwa nimekuja ili kusapoti," Don Campbell alisema baada ya kutua katika uwanja wa JKIA.

"Ndege yangu ilikuwa ndefu, sipendi safari ndefu za ndege. Lakini ilikuwa nzuri sana, ilikuwa safari ya starehe na ni furaha kuwa hapa na kusapoti pia, "aliongeza.

Staa huyo wa muziki wa reggae aliwashukuru wafuasi wake wote wa Kenya na kueleza shauku yake ya kutaka kutumbuiza nchini Kenya kwa mara ya kwanza.

Pia waandalizi wa tamasha hilo la hisani litakalofanyika KICC.

"Hii ni mara yangu ya kwanza hapa Kenya, lakini nimekuwa na kutumbuiza barani Afrika hapo awali. Hiyo ilikuwa Harare, Zimbabwe. Hiyo ilikuwa ya kufurahisha kuwa huko wakati huo. Hiyo ilikuwa miaka michache iliyopita,” alisema.

Don Campbell pia alidokeza kuwa anatazamia kukutana na mashabiki wake wa Kenya.

Mwimbaji huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la kipekee la ‘Reggae with a Cause' Wikendi ijayo

Tamasha hilo ambalo lina lengo maalum la kuwasaidia wanaoishi na ulemavu wa kutoskia litafanyika jijini Nairobi mnamo Februari 15, 2025, katika Ukumbi wa Tsavo, KICC.

'Reggea with a Cause' si tu kwa burudani ya muziki, bali pia lina lengo la kuleta mabadiliko ya kijamii, likifanya ujio wa Campbell kuwa wa kihistoria kwa mashabiki wa reggae.

Akiwa na sauti laini na nyimbo za kuvutia, Don Campbell amewashangaza mashabiki wa reggae kote ulimwenguni lakini hajawahi kutumbuiza barani Afrika—hadi sasa.

Kwenye tamasha hili maalum, anatarajiwa kushiriki jukwaa na nyota wa reggae kutoka Jamaika, Alborosie & The Shengen Clan, katika mojawapo ya matamasha makubwa ya reggae kuwahi kufanyika Kenya.

Kinachofanya tamasha hili kuwa la kipekee ni dhamira yake ya kusaidia Jamii ya Viziwi nchini Kenya.

Likiwa limepangwa kwa kushirikiana na Kituo cha Viziwi cha Kwale, tamasha hili litatoa nafasi kwa watu wasiosikia kusimamia mauzo ya chakula na vinywaji, huku washiriki wa tamasha wakipata fursa ya kujifunza na kutumia Lugha ya Alama ya Kenya.

Lengo kuu ni kubadilisha mitazamo potofu kuhusu uziwi na kuwawezesha watu wanaoish na ulemavu huu kwa kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu.

Tamasha hili pia litajumuisha wasanii maarufu wa reggae wa Kenya kama Nazizi na Wyre, pamoja na DJ wakali, likitarajiwa kuvutia watu 3,000 hadi 4,000.

Hii itakuwa fursa ya kipekee kwa mashabiki wa reggae kushuhudia msanii Don Campbell akitumbuiza Afrika kwa mara ya kwanza.

‘Reggae with a Cause’ ni mradi wa The Long Trail Community Impact, shirika la kijamii kutoka Uholanzi linalosaidia makundi yenye mahitaji maalum Afrika Mashariki.

Kwa maelezo zaidi au kushirikiana kama mdhamini, wasiliana na Jos Wesemann wa The Long Trail Community Impact kupitia barua pepe ([email protected]) au WhatsApp/Telegram (+31 6 42274229).

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved