
Mwanamziki wa Tanzania, Harmonize amefunguka na kuamua kumuomba msamaha mwanamziki mwenzake kiongozi wa Wasafi, Diamond Platinumz kutokana na post yake ya awali.
Baada ya msani Diamond kuanzisha kujenga msikiti kijiji kwa kina Harmonize, huenda halikumupendaza mwanamziki huyo
Msanii Harmonize alikuwa amendika kwenya mtandao kwamba msikiti huo ungestahili kuitwa jina halisi la Diamond ambalo ni Naseeb.
"Diamond alipatia pesa ya kuanzisha msikiti kijijini kwetu, nimeupa jina 'Masjid Naseeb," aliandika awali Harmonize.
Mwanamziki Harmonize kama njia ya kuomba msamaha kwa mwanamziki mwenzake Diamond, aliandika kwenye ukurasa wake akitaka tofauti zao zikwishe.
Harmonize aliomba msamaha moja kwa moja kwa Diamond akimtaka amuwie radhi na kujutia kutofanya hivyo mapema.
"Safari yangu ya Zanzibar imenivutia, bila shaka imekuwa kama ukumbusho kwangu kwamba maisha ya upendo ni bora zaidii. Kinamna yeyote ile sikutakiwa kurushiana maneno na ndugu yangu Naseeb [Diamond], niwie radhi ndugu yangu nisamehe. Nilichelewa kutambua hakuna mkamilifu, tuliyoyafanya pamoja ni mazuri, ni mengi kuliko shetani alie kati yetu sioni haja na faida yake," aleleza Harmonize.
Mwanamziki huyo wa Konde Gang pia kwenye ujumbe huo aliwatakia waislamu wote mwezi mtakatifu huku akiahidi kuwasamehe wote waliomkosea na kuwataka wale ambao amewakosea kupata nafasi mioyoni mwao na kumsamehe.
"Naaungana na Waisilamu wenzangu kumuomba Mungu msamaha kwa makosa yetu tulioyafanya kwa kusudia na kutokusudia. Bila shaka Mungu mwingi wa msamaha atatusamehe Insha'Allah. Kikubwa nimuombe msamaha kwa yeyote niliyemkosea kwani mimi bado nina sifa za kibinaadamu. ikiwemo kukosea. Kutoka ndani ya moyo wangu wa dhati kabisa nimemsamehe yeyote tuliyekwazana kwa lolote kupitia mwezi huu mtukufu. Nitahakikisha kila changamoto zozote nazitatua, namuomba Mungu kupitia neema ya mwezi mtukufu Ramadhani ukalete mapatano, maridhiano na kazi iendelee. kila anayesoma maandiko haya ana mchango wa aina yake katika maisha yangu," aliendelea.
Harmonize pia alifichua kwamba atakuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa mwezi huu wa tatu ifikiapo tarehe 15. Pia amekiri kwamba ni wakati wake wa kumaliza tofauti zake na watu wote akidai hazimpendezi Mungu.
"Tarehe 15 mwezi huu wa tatu inshaallah natimiza miaka 31 alihamudililahi namuomba Mungu uhai, afia pamoja na riski ninayostahili. kipekee kabisa staki kuhusishwa au kutajwa katika tofauti zozote zile kwani hazimpendezi Mungu binafsi nimezichoka," Harmonize alikamilisha maandiko yake.