
MSANII wa Konde Music Worldwide, Harmonize ameonesha nia ya kutaka kukutana na aliyekuwa bosi wake, Diamond Platnumz.
Wasanii wengi wako katika kisiwa cha Zanzibar ambapo
kunatarajiwa kufanyika hafla ya tuzo za Trace Jumatano hii.
Harmonize alikuwa na mshawasha wa kukutana na Diamond baada
ya kufika visiwani Zanzibar na kushangaa kuona msafara wa magari ya Diamond
kwenye eneo la maegesho.
Harmonize alijiuliza maswali mengi kuona magari ya Diamond
yakiwa na nambari binafsi za usajili ‘SIMBA’ huku akibaki kujiuliza ni vipi magari
hayo yaliweza kuvuka kutoka bara hadi kisiwani humo mbele ya kuwasili kwake.
Alisema kwamba kutoka kwa Diamond, amejifunza mengi, haswa
jinsi ya kufanya muziki kibiashar,a na kutaka kukutana naye wakiwa huko
Zanzibar.
“Najivunia wewe kaka
yangu. Nafikiri nimejifunza mengi kuhusu showbiz. Nawaza haya magari yamefikaje
huku. Yamepaa au yameogelea? Uko serious sana na kazi yako, ningependa kukutana
na wewe,” Harmonize aliandika.
Tamasha la kutolewa kwa tuzo hizo litafanyika katika mgahawa
mmoja kisiwani Zanzibar usiku wa leo ambapo Diamond kando na kuteuliwa kuwania
tuzo hizo, pia atakuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kabla ya kutolewa kwa
tuzo rasmi.
Wasanii wengi wa Tanzania walionesha picha na video jinsi walitua
katika visiwa vya Zanzibar, Nandy akiweka unyonge wake pembeni na kuvutia wengi
kwa jinsi alivyotua kwa ndege ya kibinafsi kabla ya kusindikizwa hotelini na
msafara mkubwa wa magari yenye haiba iliyotukuka.