
Mwanamziki Brian Ouko Omollo maarufu Khaligraph Jones kutoka hapa nchini Kenya amefichua kwamba utajiri wake wote unatokana na muziki wala hakuna mapato ya kutoka sehemu ingine.
Msani huyo ambaye anajulikana kwa muziki wake wa 'rap' amesikitikia madai kwamba hapa Kenya msanii akifaulu watu humudhania kuwa ana njia zingine za kutafuta pesa.
"Hapa Kenya kuna dhana kwamba msanii akifaulu, watu wanaamini kuna kitu kingine kinaendelea kama vile utapeli wa pesa au kazi zingine za kujificha. Lakini kila mtu ambaye ananijua anaelewa kwamba mafanikio yangu yote yanatokana na muziki pekee," alifunguka mwanamuziki huyo.
Msanii huyo mwenye umuri wa miaka 35, anajulikana kama mmoja wa wasanii wenye utajiri mwingi hapa nchini Kenya.
Jones alianza shughuli zake za kimuziki mwaka 2008 na amekuwa akishinda tuzo nyingi wakati wa kazi yake.
Aliteuliwa kuwa 'Msanii Bora wa Kiume' katika Tuzo za Afrimma za 2018, alishinda 'Msanii Bora wa Hip Hop' katika AFRIMMA za 2020, na aliteuliwa kwa 'Kitendo Bora cha Kimataifa' katika Tuzo za BET za 2020.
Aliwahi kushinda tuzo ya Channel O Music Video Awards ya Emcee Africa mwaka 2009, shindano linaloonekana sana na ambalo lilimpa sifa za kimataifa. alitoa alibam yake ya kwanza mwaka 2018 ambayo ilikuwa na nyimbo 16.
Alitajwa kuwa mwigizaji bora wa Hip Hop katika Tuzo za Soundcity MVP mnamo Januari 2020. Sherehe hiyo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Eko huko Lagos, Nigeria.
Mwanamziki huyo ambaye anajulikana kwa maisha ya starehe aliwahi kukuri kwamba jumba lake lina vyumba 'bedrooms' zaidi ya kumi.
Khaligraph ameshinda mataji mengi ambayo yamechanjia pakubwa kwenye mafanikio yake.