

Zari ambaye ni mzaliwa wa nchini Uganda kando na kuwa mwanasosholaiti pia ni mwanajamii, mfanyabiashara na mwigizaji ambaye huishi katika taifa la Afrika Kusini.
Mahakama Kuu ya Johannesburg imetoa uamuzi huo baada ya Zari kushindwa kulipa deni la ushuru linalofikia R5 milioni za Afrika kusini.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Zari anadaiwa na mlipa kodi huyo chini ya R3 milioni - sawa na Sh21,400,323 kwa kodi ya mapato ya kibinafsi, lakini kiasi hicho kiliongezeka hadi zaidi ya R5 milioni baada ya zaidi ya R2.1 kuongezwa kwenye deni.
"Kwa mujibu wa rekodi za Huduma ya Mapato ya Afrika Kusini, umeshindwa kulipa deni lako la ushuru kwa mwaka mmoja au zaidi ya kodi na vipindi vya kulipa ushuru... Unaombwa kufanya malipo kamili ndani ya siku 10 kuanzia tarehe ya barua hii ya madai," ilisomeka barua hiyo.
Katika barua hiyo, SARS ilimwagiza muigizaji huyo , ambaye pia ndie mwanzilishi wa Chuo cha Brooklyn City mjini Pretoria, kwamba ndani ya siku 10 za biashara kuanzia tarehe ya kutolewa kwa utaratibu wa kulipa deni hilo kwa awamu, ikiwa atashindwa kulipa kiasi kamili kwa wakati mmoja.
"Kushindwa kufanya malipo kamili au kutumia tiba zilizo hapo juu kunaweza kusababisha vitendo vifuatavyo na pengine vingine: Sars inaweza kuteua mtu yeyote wa tatu ambaye kwa sasa au katika siku zijazo atakudai pesa au kushikilia pesa kwako ili kutatua deni lako la ushuru la pesa hizi," barua iliandika.
Ikiwa wewe ni mtu wa asili, unaweza kuomba kupunguzwa kwa kiasi cha kulipa kwa SARS kulingana na gharama zako za msingi za maisha ya wategemezi ... Ikiwa wewe ni mtu asiye wa asili, unaweza kuomba kupunguzwa kwa kiasi cha kulipwa kwa SARS kulingana na Ugumu mkubwa wa kifedha," taarifa hiyo ilisomeka.
Zari Hassan ameolewa kwa mfanyabiashara kutoka nchini Uganda kwa jina Shakib Lutaaya.