logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto kununua mashine ya kutengeneza chapati milioni 1 kwa wanafunzi Nairobi (video)

“Sasa wewe gavana tafuta mahali ya kununua mashine ya kutengeneza chapati milioni moja,” Ruto alisema huku wanafunzi wakimshangilia.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Habari11 March 2025 - 14:22

Muhtasari


  • Kiongozi wa nchi alianza ziara yake ya maendeleo ya siku 5 katika kaunti ya Nairobi Jumatatu na alikuwa katika mtaa wa Eastleigh Eneobunge la Kamukunji.

Ruto akipakulia wanafunzi chakula

RAIS William Ruto ametoa ahadi ya kipekee kwa wanafunzi wa shule za msingi katika kaunti ya jiji la Nairobi.

Kama njia moja ya kupiga jeki mpango ulioanzishwa na gavana Sakaja wa kutoa mlo shuleni kwa wanafunzi maarufu ‘Dishi na Kaunti’, rais Ruto alisema kwamba yuko tayari kuongeza mlo wa chapati katika safu ya vyakula hivyo.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya maendeleo katika kaunti ya Nairobi, Ruto aliahidi wanafunzi kwamba atanunua mashine ya kupika chapati hadi milioni moja kwa ajili yam lo wao shuleni.

Alimtwika gavana Sakaja jukumu la kutafuta mashine hiyo ya kipekee ambayo itakuwa inapika chapati milioni moja kutosheleza idadi ya wanafunzi wanaofaidika na mpango wa Dishi na Kaunti.

“Gavana ameniuliza ya kwamba ili tuongeze chapati kwa Dishi ya Nairobi, ninunue mashine ya kutengeneza chapo (chapati), na nimekubali nitanunua mashine ya kutengeneza chapati. Sasa wewe gavana tafuta mahali ya kununua mashine ya kutengeneza chapati milioni moja,” Ruto alisema huku wanafunzi wakimshangilia.

Kiongozi wa nchi alianza ziara yake ya maendeleo ya siku 5 katika kaunti ya Nairobi Jumatatu na alikuwa katika mtaa wa Eastleigh Eneobunge la Kamukunji.

Ruto alitumia fursa hiyo ya kukutana na wananchi kupigia debe mshikamano wake mpya na kiongozi wa ODM, Raila Odinga akisisitiza kwamba kuungana kwao ni kwa ajili ya kuleta faida na maendeleo katika kila pembe ya nchi.

Baadae leo Jumanne, Ruto anatarajiwa kuzindua ujenzi wa bweni la vitanda 800 katika Shule ya Sekondari ya St Teresa’s iliyoko Mathare, eneo la mapumziko kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa katika Shule ya Msingi ya Mabatini na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Mathare Mchanganyiko.

Jumatatu, Ruto alizindua mradi wa Kukuza Upya wa Mto Nairobi, ambao alidai utafaidika takriban vijana 30,000 kutoka Nairobi kupitia ajira, kando na ujenzi wa masoko na nyumba za bei nafuu.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved