
Ni Juma ambalo tutashuhudia hatima ya majaji ikiwa kesi
mbalimbali zilizowasilishwa kortini zitasikilizwa na kuamuliwa.
Lakini hilo likisubiriwa viongozi mbalimbali walijitokeza kuwatetea majaji hao na wengeni kusema hilo si jambo la kuzungumziwa
waziwazi.
Hapo jana Jumapili, aliyekuwa naibu wa rais bwana Rigathi Gachagua
akiwa katika Kaunti ya Meru aliweza kutoa madai kwa kusema kuwa kuna mpango
unaosukwa na serikali kuwaondoa majaji saba wa mahakama ya upeo ofisini.
Katika matamshi yake Bwana Gachagua aliweza kusema kuwa ana
ufahamu wa mpango maalum ambao ulikuwa unapangwa na kuendelezwa na rais Ruto wa kuhakikisha kuwa Jaji mkuu Koome anaondolewa
afisini pamoja na majaji wengine sita.
Gachagua alionekana akimtaja kwa jina Rais Ruto akimuonya kuwa
ikiwa ataruhusu jambo kama hilo bila
shaka atakuwa amekataka uhusiano wake na watu wa mlima kenya hasa Meru
Gachagua alikuwa akiwaeleza wananchi hao kadamnasi huku akiwaahidi
kuwa iwapo rais atajihusisha na mchakato huo bila shaka atakuwa ameyakaribisha
maandano makubwa ambayo Gachagua alisema huenda atayaongoza.
Kwa upande mwingine Waziri wa usalama wa ndani Bwana Kipchumba
Murkomen alionekana kukashifu matamshi ya Gachagua akimkumbusha kuwa afisi za
majaji Pamoja na majukumu yao na adhabu inapohitajika huwa inafuata mkondo maalum tena wa kisheria ambao haupingiki na na huwa
hauingiliwi kwa misingi ya kikabila bali kwa misingi ya sheria na kazi.
Kauli ya Murkomen ilijiri punde tu baada ya Gachagua
kuzungumza akimtetea bi Koome, Murkomen alisema kuwa majaji wana njia yao ya
kikatiba na hufanya kazi kwa kuchagukiwa
bali si kwa misingi ya ukabila.
Hatimaye Naibu wa Rais Kithure Kindiki kwa namna moja pia
aliandika katika ukurasa wake wa X akisema kuwa kuondolewa kwa majai au Jaji ni
jambo la kikitiba bali si la kisiasa.
Alieleza kuwa iwapo una shida na jaji au majaji kuna tume
maalum kisheria iliyo na majukumu maalum kikatiba kutekeleza wajibu huo bali si
kulihusisha jambo hilo na ukabila ndani.
Alifafanua akisema kuwa kukosoa majaji lazima kuwe
kumejikita katika misingi ya kisheria na kwa kufuata sheria si ukabila.
Itakumbukwa vyema kuwa zipo kesi nyingi ambazo ziliwasilishwa
na wakili Havi na Ahmednasir Abdullahi wakitaka majaji hao wote waondolewe afisini kwa madai
ya usifisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.