
MREMBO mwenye umri wa miaka 25, Mercy Lavender kutoka jiji la Nakuru ni mtu mwenye mawazo mengi baada ya wazazi wake kumkasirikia kwa sababu ya kutowatumia pesa za kusherehekea Krismasi.
Lavender alipeleka masaibu yake katika kipindi cha Patanisho
kwenye Gidi na Ghost katika Radio Jambo na kusimulia jinsi wazazi wake walikata
uhusiano naye baada ya tukio hilo la Desemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa Lavender, wazazi wake walimpigia simu Desemba
24 na kumuomba pesa za Krismasi ambapo aliwaahidi kuwaombea kwa mumewe ‘hustler’
lakini hakufanikiwa kutuma.
Baadae Desemba 26, wazazi walimpigia tena wakitaka kujua nini
kilitokea hawakutuma ambapo Lavender aliahidi kufanya hivyo Januari mosi lakini
pia hawakufanikiwa.
Hapo ndipo wazazi na ndugu zake waliamua kumblock kwa pamoja
wakidai kwamba hawasaidii licha ya kumsomesha na baadae akaoleka.
“Nilikosana na wazazi
wangu Desemba, 24 babangu alinipigia akiniomba sikukuu nikamwambia ni sawa
lakini mimi sina kazi, Desemba 25-26 kufika, baba akapiga simu akaniambia
nimepanga aje nikamwambia mzee wangu amesema atatuma Januari mosi,” alisema.
“Baada ya hapo ikabidi
ameambia dada zangu waliblock akisema walinisomesha nikaoleka na siwasaidii,. Wakaniblock
wote mpaka mama hawakati stori zangu eti mimi siwapi kitu tangu nioleke na mimi
sina kazi na mzee wangu ni hustler….”
Mercy alisema kwamba kinachomsumbua sana ni laana ambazo
wamekuwa wakimtamkia na angependa kuzungumza na babake ili arudishe hayo maneno
ya laana.
“Sasa wamekuwa
wakinirushia laana nyingi sasa nikakaa nikasema wacha nipatanishwe na babangu
kwa sababu kusema ukwli mimi mwenyewe sina pesa na wamekuwa wakinirushia laana,” Mercy alisema.
Kwa upande wake mzee alipopigiwa simu, alisema kwamba ni
kweli walimkasirikia binti yake kwa sababu alikuwa amemsaidia pesa kidogo
akisema kwamba hawakukosana bali alitaka tu kunyamaza ili kumzuia asimuombe
pesa tena.
“Mimi niliona tu
ninyamaze lakini sikumwambia asikuje nyumbani. Niliwasaidia tu hadi nikaona
ninyamaze wenyewe waone vile watafanya,” mzee alisema.
Bintiye alizungumza naye akimuomba msamaha na kusema kwamba
ni vile yeye na mumewe hawana kitu na siku watakuja kupata watamsaidia.
Mzee pia aliahidi kwamba atam’unblock binti yake na kumtaka
kuacha kumpeleka mama yake mbio kwa simu.