Maafisa wa KANU walitupea milioni 10,000,000 ili kuhariri kibao cha Unbwogable-Gidi

Muhtasari
  • Tulipewa milioni 10 ili kuhariri kibao cha Unbwogable tukakataa
  • Tulitaja wanasiasa kadha wa kadha katika kibao hicho lakini hakikikuwa cha siasa
  • Familia yetu ni ya watoto kumi lakini wengi wao ni mapacha, mimi ndiye kifungua mimba
Gidi
Image: Hisani

Mtangazaji wa Radiojambo Joseph Ogidi almaarufu Gidi ameeleza jinsi walivyo lipwa milioni kumi ili kuimba wimbo wakisifu chama cha siasa cha KANU.

Kibao cha unbwogable kilifahamika sana, huku msanii Majimaji na Gidi wakikataa pesa hizo.

Akiwa kwenye mahojiano Gidi alieleza jinsi muziki na utangazaji umebadilisha maisha yake, mnamo mwaka wa 2008 Gidi alijiunga na Radiojambo ambapo amekuwa akifanya kkipindi cha asubuhi cha 'Gidi na ghost' huku akisaidiwa na mwenzake Ghost Mulee.

 

" Nilimpigia maji aje kunisaidia kurekodi kibao cha unbwogable, aliniuliza hiyo ni nini,mnamo mwaka wa 2002 tulienda studio na kurekodi kibao hicho

Katika kibao hicho, tulitaja majina kdhaa ya wanasiasa lakini hakikuwa kibao cha siasa, maafisa wa KANU walikuja na kutupa milioni 10 ili tubadilishe mistari ya kibao hicho ambapo alituambia tunapaswa kusifu cham cha KANU lakini tulikataa

Wakati huo pesa nying ambazo tulikuwa tumeshika ni elfu 100,000." Alieleza Gidi.

Baada ya iki moja kibao hicho kilikuwa kimefahamika sana kwenye mitandao ya kijamii.