Kutana na wacheza santuri ambao wana mshahara mkubwa nchini kenya

Muhtasari
  • Nchi ya kenya imebarikiwa na wacheza santuri tofauti wa nyimbo tofauti
  • Wacheza santuri hao wana weledi wa kipekee, na huwa wanapokea mapato mema katika kazi yao
Dj-Joe-Mfalme-700x466
Dj-Joe-Mfalme-700x466

Wacheza santuri ndio huwafurahisha mashabiki wao kwa weledi ambao wanao wa kucheza nyimbo tofauti.

Kuna wale wamo safarini ya kuwa DJ maarufu maishani, na pia kuna wale waliachia kazi katikati na kusema wacha kazi hiyo ikae kwa maana si kazi rahisi kama vile wanavyoona.

Nchi ya kenya imebarikiwa na wacheza santuri tofauti wa nyimbo tofauti kama  za injili,reggae,secular miongooni mwa nyingine.

 

Pia kuna wacheza santuri wanawake na wanawake, katika makala haya tutaangazia wacheza santuri ambao wanamshahra mkubwa nchini.

Hii hapa orodha ya baadhi ya wacheza santuri ambao wanapokea kipato kikubwa endapo atawaburdisha mashabiki kwa hafla moja au nyi ngine.

1 DJ Joe Mfalme

Hivi majuzi Joe alitoka kwenye redio ya Capita na kujiunga na kampuni ya Radio Afrca, katika redio ya Homeboyz.

Katika kila hafla mcheza santuri huyo hupokea shillingi elfu 180,000.

2.DJ Mo

Mo anafahamika kila mahali nchini kenya, hupokea mshshara wa shillingi elfu 150,000 katika hafla ambayo ataalikwa kuwaburudisha mashabiki.

 

3.DJ Pierra Makena

Ni mcheza santuri wa mwanake ambaye ana bidii katika kazi yake, hupokea shillingi elfu 150,000 katika kila halfla ataalikwa.

4.DJ Kalonje

Katika nyimbo za reggae mcheza santuri huyo amebarikiwa na ana kipaji cha kipekee hupokea shillingi elfu160,000 katika kila hafla atakayo alikwa kucheza santuri.

5.DJ Creme de la creme

Hupokea shillingi elfu 16,000.

Miongoni mwa wacheza santuri wengine ni kama vile DJ Nick Dee mioongoni mwa wengine.