Mambo ambayo hustahili kumwambia mwanamume unayempenda

Muhtasari
  • KIla mwanamume hupenda familia yake iwe na furaha na hata kutia bidii ili atimize mahitaji ya familia yake
  • Mambo ambayo hustahili kumwambia mwanamume unayempenda
sad woman
sad woman

Kuna mambo meni ambayo hustahili kufikiria kumwambia mwanamume ambaye unampenda, kwa maana ataumia moyo bali hatakuambia kwamba umemuumiza kwa maneneo yako.

Wanawake wengi hubaki na mshangao kwanini uhusiano wao au mpenziye hana hisia zake kamwe na kushindwa kosa ambalo alifanya kumbe maneno yako yamemsukuma mbali nawe.

Haya hapa mambo ambayo hustali kumwambia mwanamume unayempenda.

 

1.Unatamani hungepatana naye

Ndio endapo umepatana na mtu maishani mwako kuna sababu nzuri au mbaya, na kati ya sababu hiyo mbaya utajifunza kutoka kwa hilo.

Kama unampenda mwanamume yeyote na mumeanza kubishana au kukeleleshana, kuwa makini na neno kuwa unatamani hungepatana naye maishani mwako au wajuta kumpenda.

2.Fulani na ulani ni bora kukuliko

Wanawake wengi wana tabia ya kuwwalinganisha waume zao na wengine has wale hawajafaulu maishani hupata msoo kutoka kwa wanawake wao kila siku.

Kama unataka mume au mpenzi wako akupende haya basi toa neno la kumfananisha na rafiki zake au mtu mwingine yeyote.

KIla mwanamume hupenda familia yake iwe na furaha na hata kutia bidii ili atimize mahitaji ya familia yake.

 

3.Pole lakini..

Kama umemkosea mwanamume wako muombe msamaha lakini usiweke lakini katia msamaha wako au kulaumu kwa yote ambayo yametokea katika uhusiano wenu.

4.Najaribu kuishi na wewe

Hilo linauma sana kumwambia mwanamume kwamba unajaribu kukaa naye, haya yanaonyesha kwamba huna hisia zake kamwe.

5.Sijawahi kuwa na hisia zako

Kama hujawahi kuwa na hisia zake unafanya nini katika uhusiano huo au ndoa hiyo? ata kama umekassirika kiasi kipi toa manaeno hayo kwenye mdomo wako.

Hawakukosea waliposema ulimi kiungo kidogo lakini kina madhara makubwa.