Orodha ya marais wa Afrika walioaga dunia wakiwa mamlakani

Muhtasari
  • Orodha ya marais wa Afrika walioaga dunia wakiwa mamlakani
  • Wengi waliombolezwa kwa nia tofauti, huku wengi wakiacha pengo kubwa serikalini
Marehemu rais John Pombe Magufuli
Marehemu rais John Pombe Magufuli

Afrika kwa muda sasa imewapoteza marais ambao wamekuwa mamlakani kwa muda mrefu na hata wameaga ama waliaga dunia wakiwa mamlakani.

Vifo vya baadhi ya marais hao viliwashtua wengi na wananchi kwa jumla.

Wengi waliombolezwa kwa nia tofauti, huku wengi wakiacha pengo kubwa serikalini.

 

Hii hapa orodha ya marais wa Afrika ambao waliaga dunia wakiwa mamlakani;

1.John Pombe Magufuli

Hayati Magufuli aliaga dunia Machi 17 2021 kutokana na matatizo ya moyo, mwendazake alikuwa rais wa tano wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

2.Pierre Nkurunzinza

Pierre aliaga dunia mwaka wa 2020 8 JUni, alikuwa ametawala nchi ya Burundi kwa miaka 15.

3.John Evans Fiifi

Alikuwa rais wa Ghana, ambaye aliaga dunia akiwa mamlakani, hayati aliaga dunia  julai,24,2012, Evans aliaga dunia akipokea matibabu.

 

4.Michael Sata

Aliaga dunia mwaka wa 2014, Oktoba  alipokuwa anapokea matibabu nchini London, alikuwa rais wa tano wa nchi ya Zambia.