Mwanasosholaiti chipukizi Manzi wa Kibera amuomba mama yake msamaha

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti chipukizi Manzi wa Kibera alifahamika baada ya kudai kwamba mwanasosholaiti Shakilla alichukua 'Sponsor' wake
  • Baada ya mwanasosholaiti kuona hadithi ya mama yake, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemuomba msamaha kwa yale amekuwa akifanya

Mwanasosholaiti chipukizi Manzi wa Kibera alifahamika baada ya kudai kwamba mwanasosholaiti Shakilla alichukua 'Sponsor' wake.

Mama yake ambaye amemlea akiwa kwenye mahojiano, alisema kwamba alikuza Manzi wa Kibera kwa njia za Mungu hadi pale alibadilika na kumkana na kusema kwamba yeye sio mama yake tena.

Huku akieleza jinsi alimkuza baada ya mama yake mzazi kuaga dunia alikuwa na haya ya kusema,

 

"Nilianza kumlea wambui, alipokuwa na mika miwili baada ya mama yake kuaga dunia, tumeishi Limuru naye

tulikosana naye baada ya kuona picha zake akionyesha uchi wake, nilipomuuliza alitoroka na kuniambia kwamba mimi sio mama yake, n kwamba mama yake alikufa

Nimemlea kwa kanisa, alifika kidato cha kwanza kwa maana sikuwa na uwezo wa kumpa masomo, kwa maana nina watoto wengine

nilimuona akiwa na tabia tofauti, anavaa nguo fupi na mimi sipendi hayo," Alizungumza.

Baada ya mwanasosholaiti kuona hadithi ya mama yake, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemuomba msamaha kwa yale amekuwa akifanya.

Manzi wa KIbera alipakia video ya mama yake akiwa kwenye mahojiano na kuandika ujumbe huu;

"Pole maa," Aliandika.

Mshabiki wake walimpongeza kwa kuomba mama yake msamaha.