Njia ya muongo ni fupi,' Mkewe msanii Rayvanny amkashifu msanii huyo

Muhtasari
  • Mkewe Rayvanny amkashifu msanii huyo kwa kuitema familia
  • Mama huyo aliweka wazi kwamba ametosha kudanganywa,na kwamba njia ya muongo ni fupi

Fahima, aliyekuwa mkewe msanii wa Bongo Rayvanny hatimaye ameweka wazi kwamba wawili hao wameachana huku akidai kwamba msanii huyo amekuwa muongo.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram mama huyo alisema kwamba amesalia tu na mwanawe licha ya msanii huyo kuwa tajiri.

Kupitia kwa jumbe zake alisema kwamba Rayvanny alikuwa amesahau na familia yake nakuwa njia ya muongo ni fupi.

 

"Tajiri na mali yake, maskini na mwanae malipo ni hapa duniani,"

Katika ujumbe mwingine aliharifu msanii huyo kwamba ameharibu familia yake kwa mikono yake mwenye na ipo siku Mungu atamkumbusha.

Ujumbe wake mwingine ulisoma;

"Nimekubalu kutukanwa,kubeba maumivu yote nikijua navumilia kwa mtu ambae najua ni wa muhimu kwangu kumbe najidanganya mwenyewe

Imetoshaa sasasiwezi tenaa endelea na huu mchezo ambao hauna mwisho sitaki," Aliandika Fahima.

Mama huyo aliweka wazi kwamba ametosha kudanganywa,na kwamba njia ya muongo ni fupi.

"Nasema tena kuwa njia ya muongo ni fupi,mtakapo sikia ukweli kutoka kwangu kila mtu ata wachukia wanaume,"