Umetuangusha,nataka 500 yangu,'Manzi wa Kibera amwambia Omosh

Muhtasari
  • Manzi wa KIbera asema amesikitishwa na hatua ya Omosh
Manzi wa KIbera
Image: maktaba

MuigizajiJoseph Kinuthia maarufu Omosh siku ya Ijumaa alivuma mitandaoni baada ya kuomba wakenya msaaa tena.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram mwanasosholaiti huyo chipukizi alifichua kwamba alimtumia Omsh mia tano na anahitaji pesa zake.

"Mimi mwenyewe nilimtumia Omosh mia tano, na nina jumbe za M-pesa  na nataka mia tano yangu tena,"

Aliendelea na ujumbe wake na kumwambia muigiaji huyo aseme ukweli, na kuwa ameangusha wale wote ambao walimsaidia wakati alipokuwa anahitaji msaada wao.

"Watu kaa mimi na wakenya tukakuchangia, nakumbuka nilikuchangia mia tano,niliibariki na nikasema ikusaidie

Watu kama Jalang'o walikusaidia sana unataka kusema alikula hizo pesa zako ama anadanganya, mwanasaiasa Alinur pia alikusiada

Omosh ongea tu ukweli,mimi kama Manze wa KIbera na wakenya wote ambao walikuchangia tumesikitika sana ata kama ni mwenye alikucangia shilingi kumi

Umetuumiza yaani umetuangusha," Alisema Manzi wa Kibera.

Sio Manze wa KIbera tu ambaye amemkashifu Omosh bali baadhi ya wakenya wamesikitishwa na hatua ya Omosh.

Huku akijibu madai hayo Omosh alisema kwamba pesa huisha na kuwa hakuwa analazimisha mtu yeyote kumtolea pesa kwa mara ya pili.