Nameless,Wahu na Sauti Sol wamekuwa wakinitafuta tufanye collabo-Ghost Mulee

Muhtasari
  • Fahamu kwa nini msanii Nameless, Sauti Sol wamekuwa wakimtafuta mtangazaji Ghost
Ghost Mulee

Wasanii wa humu nchini wamekuwa wakifanya collabo na wasanii tofauti wa humu nchini na wengine wa nchi za nje.

KIla msanii amekuwa akitia bidii katika kazi yake kwa kutoa kibao kimoja baada ya kingine hasa wakati huu wa janga la corona.

Baada ya corona kuingia nchini mwaka jana Machi, baadhi ya wasanii walionekana kufifia katika usanii wao.

Siku ya Jumanne wakati wa kipindi cha asubuhi cha Gidi na Ghost asubuhi, mtangazaji Mulee alifichua kwamba wasanii kama Nameless, Sauti Sol wamekuwa wakimtafuta ili watoe collabo naye.

Haya yalijiri baada ya Ghost kuimba kibao kimoja na Gidi kumtania na kumwambia kwamba hana sauti ya kuimba.

"Wewe hujabarikiwa na sauti ya kuimba, lakini maneno uko nayo," Gidi alimtania Ghost.

Ghost alikuwa na haya ya kumwambia mwenzake;

"HUjui akina Sauti Sol, Nameless, Wahu wamekuwa wakinitafuta tufanye collabo na wao," Ghost naye alimtania Gidi huku akicheka.

Je kulingana na maoni yako Ghost ana sauti ya kuwa msanii au la?