'Usianike uhusiano wako wa kimapenzi mitandaoni,' Ujumbe wa Burale kwa mashabiki

Muhtasari
  • Msemaji maarufu wa motisha Robert Burale amewashauri wanamitandao kuacha kuanika uhusiano wao kwenye mitandao ya kijamii
Robert Burale
Robert Burale

Msemaji maarufu wa motisha Robert Burale amewashauri wanamitandao kuacha kuanika uhusiano wao kwenye mitandao ya kijamii.

Kulingana na Burale, mitandao ya kijamii ina kila aina ya watu wanaoishi maisha yao na kwa hivyo haiwei kuwa salama kwa uhusiano unaochipuka.

Kocha huyo wa maisha alisema ikitokea kuachana, wenzi hawapaswi kuwa na tabia ya kuumizana kupitia mitandao ya kijamii.

"Usichukuliwe na "wapendao" na "wafuasi" kwenye mitandao ya kijamii .... Nafasi yake ni "bandia" kubwa .. Ikiwa mitandao ya kijamii inakupa kitambulisho basi unahitaji kujirudia na kujitafuta

 Usifanye maamuzi kulingana na mitandao ya watu wengine "mafanikio" Usitangaze uhusiano wako kwenye mitandao ya kijamii kabla mizizi haijatua ardhini ... ni eneo la vita huko nje ... Usianze kudhalilishana kwenye mitandao ya kijamii wakati mnavunjika ... "ujinga"Alisema Burale.

Alielendeea na ujumbe wake huku akidai kwamba hali ya akili ya kila mmoja lazima ilindwe.

" Mitandao ya kijamii ina watu wa kila aina .. wazuri .. wazimu ... nk .. usichukue chochote kibinafsi ..Tumia kitufe cha kuzuia ikiwa lazima ... Hali yako ya akili lazima ilindwe ," Alisema.

Sio mmoja au wawili bali tumeona baadhi ya watu mashuhuri wakianika uhusiano wao wa kimapenzi mitandaoni, huku baadahi yao wakiachana pia wanatangaza kutpitia kwenye kurasa za za mitandao ya kijamii.