'Nakupenda,'Vyette Obura na Bahati washerehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao

Muhtasari
  • Vyette Obura na Bahati washerehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao
Vyette Obura na mwanawe
Image: INSTAGRAM/Bahati

Vyette  Obura na Bahati kupitia kwenye  kwenye kurasa zao za instagram instagram walisherehekea siku ya kuzaliwa  kwa binti yao.

Yvette alisherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye kwa kuweka picha nzuri kwenye instgram yake na kumshukuru Mungu kwa hatua waliyofikia.

“Tumefanikiwa kufika kwenye big 6 kwa neema ya Mungu happy birthday to my not so little beautiful baby I love you so much.” Yvette aliandika ujumbe huo wa hisia.

Bahati ni baba wa bintiye Yvette na wamekuwa wakimlea binti yao na kiukweli kabisa wanaonekana kufanya kazi nzuri kwani hakujawa na malalamiko juu ya Bahati kuwa 'deadbeat dad' au kumtelekeza binti yao.

Bahati pia alimshukura Vyette kwa kuwa mama bora kwa binti yake, na huu hapa ujumbe wake;

"HERI YA SIKU YA 6 YA KUZALIWA BINTI YANGU @MUENI_BAHATI 💗 Na ninapomshukuru Mungu kwa Kipaji, Uzuri na Ukuaji Wako; Ningependa pia kumshukuru Mama Yako Yvette kwa Kuwa Mama Bora Unayoweza Kumuuliza au Kumuombea!

Ombi langu ni kwamba Mungu Akupe Afya Kamili na Mafanikio. Nikukumbushe tu kwamba Una maana só Mengi kwangu na nitafanya kila niwezalo kuwa Baba Bora katika Ulimwengu Wako. Furahia Siku Yako ya Kuzaliwa Princess 💗 @Mueni_Bahati," Aliandika Bahati.